Serikali ya Tanzania yapata tuzo kutoka WHO
Shirika la Afya Duniani (WHO) limeipa tuzo Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya katika jitihada zake za kupambana na ugonjwa wa malaria.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kupokea tuzo hiyo jana Jumatatu Februari 26, 2018, Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohammed Bakari amesema matukio ya wagonjwa wanaougua malaria yamepungua kwa kiasi kikubwa.
Kwa upande mwingine Bakari amesema kudhibiti malaria kwa watoto wa chini ya miaka mitano ni mafanikio makubwa kwa sekta ya afya nchini.
Aidha, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la WHO nchini, Dkt. Rita Njau amesema tuzo hiyo imetolewa kwa Tanzania baada ya kufanikiwa kupunguza maambukizi ya malaria kwa kipindi cha miaka 10.
“Kumekuwa na mafanikio kwa maana ya mwaka 2008 kwa matukio ya wagonjwa wa malaria ambayo yaliripotiwa yalikuwa milioni 18, mwaka 2017 namba hiyo imepungua na kuwa ni milioni 5.5, haya ni mafanikio makubwa sana katika udhibiti wa malaria nchini,” amesema Prof. Bakari.
Kwa upande mwingine Bakari amesema kudhibiti malaria kwa watoto wa chini ya miaka mitano ni mafanikio makubwa kwa sekta ya afya nchini.
“Takwimu za mwaka 2008 zinaonyesha kuwa vifo vya watoto chini ya miaka mitano vilikuwa ni 112 kati ya watoto 1,000 na mwaka 2017 tunaona vifo vimepungua mpaka kufikia 67 kwa watoto 1,000, hii inaonyesha mafanikio makubwa katika maendeleo ya kudhibiti malaria,” amesema Prof Bakari.
Aidha, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la WHO nchini, Dkt. Rita Njau amesema tuzo hiyo imetolewa kwa Tanzania baada ya kufanikiwa kupunguza maambukizi ya malaria kwa kipindi cha miaka 10.
Serikali ya Tanzania yapata tuzo kutoka WHO
Reviewed by Zero Degree
on
2/27/2018 08:37:00 AM
Rating: