Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 22 Februari, 2018

Luka Modric 
Luka Modric ataondoka Real Madrid kwenye majira ya joto kama klabu hiyo ya Uhispania itatwaa taji Ligi ya Mabingwa kwa mara ya tatu mfululizo.

Beki wa klabu ya Barcelona, Samuel Umtiti hafurahii mkataba wake wa sasa katika klabu hiyo na tayri Manchester United imeonyesha nia ya kutaka kumsajili  Mfaransa huyo.

Golikipa wa klabu ya Manchester United, David de Gea amewaambia marafiki zake kwamba, Jose Mourinho yuko tayari kumruhusu aende Bernabeu mwisho wa msimu huu, kama Madrid watakubali kumwachia kiungo wa Ujerumani, Toni Kroos kama sehemu ya makubaliano. (Don Balon)

Kevin De Bruyne anahusishwa na uhamisho kwenda Real Madrid kwenye majira ya joto.

Klabu ya Chelsea inatazamia kumsajili kiungo wa klabu ya Real Madrid, Marco Asensio mwishoni mwa msimu huu.

Rais wa Bayern Munic amekuna na kufanya mazungumzo na kiungo wa klabu ya Juventus, Sami Khedira juu ya kurejea nchini Ujerumani kwa Mabingwa hao wa Bundesliga.

Thibaut Cortouis anaweza kuachana uhamisho kwenda Real Madrid na kuamua kusaini mkataba mpya katika klabu ya Chelsea. (ESPN)

Klabu ya Real Madrid inataka golikipa wa Chelsea Thibaut Courtois achelewe kusaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Uingereza hadi mwezi Aprili ambapo watafanya uamuzi wa kumsajili raia huyo wa Ubelgiji au David de Gea wa Manchester United . (Telegraph) 

Harry Maguire
Beki klabu ya Leicester City na Timu ya Taifa ya Uingereza, Harry Maguire yuko tayari kumaliza soka lake katika klabu hiyo, licha ya kuhusishwa na uhamisho kwenda klabu ya Manchester City. (Sun)

Leon Bailey amevunja ukimya juu ya tetesi zinazomhisha na uhamisho kwenda Arsenal, Chelsea na Manchester United kwa kusema kuwa kwa sasa Bayer Leverkusen ndio mahala sahihi kwake na hana raka ya kukimbilia uhamisho kwenda katika vilabu vikubwa.

Wakala wa kiungo wa Paul Pogba amempa ofa mteja wake achague klabu kubwa anayopenda kuitumikia baada ya hali ya maelewano baina yake na Jose Mourinho kuzidi kuwa mbaya.

Chelsea inamfukuzia winga wa klabu ya Borussia Dortmund, Christian Pulisic aje kuchukuwa nafasi ya Eden Hazard kama ataondoka kwenda Real Madrid.

Nikola Moro
Manchester United ina matamanio makubwa ya kumsajili kiungo wa kati wa klabu ya Dinamo Zagreb, Nikola Moro. (Talksport)

John Evans atarejea kwenye nafasi ya unahodha katika klabu ya West Brom siku ya Jumamosi wakati timu yake itakapocheza dhidi ya Huddersfield.

Zinedine Zidane anasema kuwa atapigana vilivyo kulinda kibarua chake kama meneja wa kalbu ya Real Madrid.

Craig Bellamy amefanya mazungumzo na klabu ya Oxford united, na anaweza kuthibitishwa kuwa kama meneja mpya wa klabu hiyo wiki ijayo. (Sky Sports)

Klabu ya West Bromwich Albion inamfuatilia meneja wa klabu ya Ostersunds, Graham Potter.

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger anamtaka mshambuliaji Danny Welbeck, asaini kandarasi mpya na klabu hiyo ya London. (Daily Mail)

Kiungo wa klabu ya Lyon, Mohamed Bahlouli anahusishwa na uhamisho kwenda Liverpool kwenye majira ya joto.

Davinson Sanchez
Beki wa klabu ya Tottenham na Timu ya Taifa ya Clombia, Davinson Sanchez, ambaye alijiunga klabu hiyo mwezi Agosti 2017 kutoka Ajax, anasema kuwa hapendelei kuuhamia Real Madrid mwisho wa msimu huu.. 

Wakala wa Golikipa wa klabu ya Chelsea
 atasikiliza ofa kutoka Real Madri, licha ya kwamba raia huyo wa Ubelgiji amesema anafurahia kuwa Chelsea. (Mirror)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 22 Februari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 22 Februari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 2/22/2018 10:45:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.