Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 23 Februari, 2018

Golikipa wa Manchester United, David de Gea
David de Gea anatarajiwa kuongeza mkataba wake katika klabu ya Manchester United, ikiwa na maana kwamba Real Madrid watarejesha nguvu zao kwa kipa wa Chelsea Thibaut Courtois.

Tottenham iko tayari kumuuza beki wake, Toby Alderweireld kwenye majira ya joto akiwa na mtamanio ya kulipwa mshahara wa pauni 150,000 kwa wiki, hiyo ikiwa na maana kuwa mazungumzo yamekosa mwafaka.

Lakini Spurs wana uhakika kuwa Jan Vertonghen atasaini mkataba mpya wa mwaka mmoja - wakati mkataba wake wa sasa utakapoisha mwishoni mwa msimu ujao. (Times)

Bolton imekamilisha usajili wa aliyekuwa nyota wa klabu ya Sunderland, Jan Kirchhoff.

Arsene Wenger ndiye anayeikwamisha klabu ya Arsenal, kwa mujibu wa Mathew Syed.

Beki wa klabu ya West Ham, Jose Fonte anakaribia kujiunga na klabu ya Dalian Yifang ya China.

Askari Polisi afariki dunia baada ya kupata mshtuko wa moyo kufauatia ugomvi ulioibuka kati ya mashabiki wa Athletic Bilbao na Spartack Moscow kabla ya mechi yao ya Europa Ligi. (Sky Sports)

Jose Mourinho yuko tayari kutafuta amani na kati yake yeye na Antonio Conte siku ya Jumapili.

Eddie Jones amesema kuwa alikuwa shabiki wa West Ham tangu utotoni - lakini anataka timu yake ya Uingereza icheze kama Manchester City.

Sergio Aguero hatamshtaki shabiki wa klabu ya Wigan ambaye aligombana naye baada ya Manchester City kuondolewa kwenye FA Cup.

Raheem Sterling
Raheem Sterling ametilia shaka future yake katika klabu ya Manchester City - na hilo litaifanya Real Madrid ikae mkao wa kula. (Mirror)

Muda wa mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Wales, Gareth Bale katika klabu ya Real Madrid unaelekea ukingoni.

Neymar lazima aondoke PSG ajiunge na klabu ya Real Madrid, kwa mujibu wa aliyekuwa kiungo wa Madrid, Gutti.

Michy Batshuayi amedai kuwa mashabiki wa klabu ya Atalanta walimwimbia nyimbo za kibaguzi wakati wa mchezo kati ya Timu hiyo ya Italia na Borussia Dortmund kwenye Ligi ya Europa. 

Beki wa klabu ya Real Madrid, Alvaro Arbeloa amemkingia kifua Gareth Bale kwa kusena kuwa vigogo hao wa La Liga wasimuuze straika huyo. (ESPN)

Klabu ya Chelsea inafanya mpango wa kumnasa beki wa Newcastle, Jamaal Lascelles (London Evening Standard)

Shirikisho la Soka la Uingereza litashindana na Uskoti kuhakikisha kiungo wa Manchester United, Scott McTominay anaichezea Timu ya Taifa ya Uingereza.

Mmiliki wa klabu ya Sunderland, Ellis Short ataitoa klabu hiyo bure kama mnunuaji atakuwa tayari kulipa deni kubwa ambalo klabu hiyo inadaiwa.

Gabriel Jesus ameonekana akifanya mazoezi kwa mara ya kwanza tangu arejea atoke majeruhi.

Wachezaji wa Cardiff City watapewa bonasi ya pauni milioni 10 wagawane kama watafanikiwa kuipandisha daraja timu hiyo hadi Ligi Kuu ya Uingereza.

Mtoto wa Kevin Campbell, Tyrese anaweza kucheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu ya Uingereza akiwa na klabu ya Stoke City siku ya Jumamosi, Paul Lambert akifikiria kumjumuisha mshambuliaji huyo chipukizi kikosi cha siku hiyo. (Daily Mail)

Meneja wa Manchester United,  Jose Mourinho
Mimi ndio bosi hapa, Jose Mourinho alimwambia Paul Pogba wakati wakiwa mazoezini.

Angel Gomes na Ethan Hamilton wameongezwa kwenye kikosi cha Manchester United cha Ligi ya Mabingwa.

Pep Guardiola anakaribia kusaini mkataba mpya Manchester City utakaoisha mwaka 2021.

Yannick Carrasco aliachwa nje ya kikosi cha Atletico Madrid kilichoenda nchini Denmark kucheza dhidi ya FC Copenhagen kwenye Europa Ligi, Mbelgiji huyo akikaribia kutimkia China. (Sun)

Barcelona, Bayern Munic na Liverpool zitashindania saini ya winga wa klabu ya Sporting Lisbon, Gelson Martins.

Brendan Rodgers ataifaa sana klabu ya Tottenham kama Maurcio Pochettino ataamua kuondoka. (talkSport)

Paul Pogba anatambua kuwa Jose Mourinho amaemfanya aonekane kama mwenye nguvu ndani ya kikosi cha Manchester United. (Express)

Klabu ya Atletico Madrid inatazamia kusajili chipukizi wa klabu ya West Ham, Reece Oxford, ambaye anaichezea Borussia Monchengladbach kwa mkopo kwenye majira ya joto.

Raheem Sterling hajaambiwa na klabu ya Manchester City ni lini mazungumzo juu ya mkataba mpya kati yake na klabu hiyo yatafaanza. (Telegraph)

Sergej Milinkovic-Savic
Manchester City na Manchester United zinategemewa kushindania saini ya kiungo wa klabu ya Lazio, Sergej Milinkovic-Savic. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 23 Februari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 23 Februari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 2/23/2018 10:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.