Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 3 Februari, 2018

Golikipa wa klabu ya Manchester United, Davi de Gea
Jose Mourinho yuko tayari kumruhusu David de Gea ajiunge na Real Madrid kama atampata Gareth Bale kama sehemu dili lao.

Meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp ameisifu klabu ya Tottenham kwa kuwabakisha wachezaji wake wazuri. (Star)

Msambuliaji wa West Ham, Javier Hernandez anakiri kwamba aliiomba klabu yake iangalie kama kuna uwezekano wa yeye kuhama mwezi Januari lakini ameapa kuitumikia klabu hiyo kwa moyo wote kam ilivyokuwa siku zote.

Klabu ya Leicester City haitambui ni Riyad Mahrez atarejea mazoezini kufuatia kgoma kumruhusu ajiunge na Manchester City.

Hatimaye Arsene Wenger amekiri kwamba alifanya makosa makubwa sana kuacha kumuuza Alexis Sanchez kwa pauni milioni 60 kwenye majira ya joto mwaka 2017. (Mirror)

Meneja wa klabu ya Everton, Sam Allardayce amesema kuwa klabu ya Arsenal iliamua kumuuza Theo Walcott kwa bei nafuu kwa nia njema baada ya nyota huyo kuitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu.

Meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp
Jurgen Klopp anasema kuwa kumaliza katika nafasi nne bora kwenye Ligi Kuu ya Uingereza itakua ni mafanikio kwa Liverpool msimu huu. (Telegraph)

Crystal Palace imekubali kumsajili olikipa wa klabu ya Getafe, Vicente Guaita hata hivyo, hataweza kujiunga na klabu hiyo hadi mwezi Julai.

Leicester inafuatilia kwa karibu juu ya sakata la Daniel Opare na klabu yake ya Augsburg.

Maelfu ya mashabiki wa klabu ya West Ham wanampango wa kuandamana kupinga bodi ya klabu hiyo kabla ya mechi yao dhidi ya Burnley mwezi Machi.

Ronald Koeman anatarajiwa kutangazwa kuwa meneja wa timu ya taifa ya Uholanzi. (Sun)

Leicester haikutaka kumuuza Islam Slimani kwenda West Ham kwa sababu Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Uingereza 2015/16 bado wana hasira kufuatia maoni ya Karren Brady.

Pep Guardiola anawapa nyota wa Manchester City siku nne za mapumziko, klabu hiyo ikielekea kunyakua taji la Ligi Kuu ya Uingereza. (Daily Mail)

Chelsea imepeta pigo katika harakati za kumtafuta mrithi wa Antonio Conte, baada ya Diego Simeone kuweka wazi kwamba hategemei kuwa meneja wa klabu hiyo.

Wachezaji wa Leicester City hawafurahii mpango wa klabu yao kutaka kumrejesha Riyad Mahrez kikosini baada ya winga huyo kuacha kuhudhuria jana na kujitenga na klabu yake kwa siku ya tatu mfululizo. (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 3 Februari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 3 Februari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 2/03/2018 10:38:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.