Loading...

Zitto Kabwe aomba kampeni za uchaguzi mdogo zisimamishwe kwa muda wa siku 3


Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, ameviomba vyama vya Chadema na CCM kusimamisha kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani kwa siku tatu kuomboleza kifo cha Mzee Kingunge Ngombale Mwiru.

Zitto Kabwe ametoa kauli hiyo akiwa kwenye msiba wa Mzee Kingunge nyumbani kwake Kijitonyama, Dar es Salaam, na kusema kwamba sio busara kwa wao kuendelea na kampeni wakati Kingunge amesaidia kuviimarisha vyama hivyo,

"Sasa hivi kuna kampeni zinaendelea kwenye jimbo la Kinondoni, na bahati nzuri Mzee Kingunge ameasisi CCM na amesaidia shughuli za kisiasa za CHADEMA. Sioni busara vyama kuendelea na kampeni. Nawaomba wasitishe leo, kesho na Jumatatu mwanasiasa huyu akizikwa wataendelea na kampeni" amesema Zitto Kabwe.

Mzee Kingunge Ngombale Mwiru nchi inamtambua kama mwanasiasa mkongwe wa nchi ambaye ameshiriki kukijenga chama cha CCM kwa miaka mingi mpaka pale alipokihama chama hiko mwaka 2015.

Mzee Kingunge amefariki dunia Februari 2 akiwa hospitali ya Muhimbili alikolazwa akipatiwa matibabu, na anatarajia kuzikwa Februari 5, katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam
Zitto Kabwe aomba kampeni za uchaguzi mdogo zisimamishwe kwa muda wa siku 3 Zitto Kabwe aomba kampeni za uchaguzi mdogo zisimamishwe kwa muda wa siku 3 Reviewed by Zero Degree on 2/03/2018 10:03:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.