Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 10 Februari, 2018

Alexandre Lacazette 
Muda wa Alexandre Lacazette katika klabu ya Arsenal tayari umekwisha, kwa mujibu wa Emmanuel Petit.

Arsenal inaweza kutibua mipango ya Chelsea kwa kumnasa aliyekuwa meneja wa klabu ya Barcelona, Luis Enrique achukue nafasi ya Arsene Wenger.

Klabu ya Manchester United ndio imepewa nafasi kubwa ya kufanikiwa kumnasa winga wa Borussia Dortmund, Christian Pulisic. (Sun)

Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane amekanusha taarifa zinazodai kuwa klabu hiyo ina mpango wa kumuuza Isco kwenye majira ya joto.
 
David Moyes amekubali kufanya mazunguzo na klabu ya West Ham juu ya mkataba mpya kwenye majira ya joto.

Islam Slimani anaweza kupewa mkataba wa kudumu katika klabu ya Newcastle kama ataisaidia klabu hiyo isishuke daraja.

Javier Hernandez amesema kuwa klabu yake ya West Ham imefanya jambo jema sana kwa kumsajili Patrice Evra.

Xherdan Shaqiri ana hamu ya kupigana kuisaidia klabu ya Stoke City isishuke daraja, kwa mujibu wa meneja wa klabu hiyo, Paul Lambert. (Sky Sports)

Manchester City imekubali kulipa ada ya karibuni sawa na pauni milioni 44.5m kumsajili kiungo wa Shakhtar Donetsk, Fred.

Manchester United na Manchester City zinatarajiwa kushindania saini ya beki wa Leicester, Harry Maguire.

Pep Guardiola amemtaja Kevin De Bruyne kama mmoja wa wachezaji wenye kipaji kuwahi kumuona katika maisha yake na mfano mzuri kwa Manchester City.

Klabu ya Norwich City itahitaji kiasi cha pauni milioni 30 kumruhusu kiungo wao, James Maddison aondoke kwenye majira ya joto, baada ya kukataa kumuuza nyota huyo aliyekuwa anawaniwa na Liverpool na Tottenham mwezi Januari.

Aliyekuwa mshambuliaji wa Arsenal, Marouane Chamakh bado anasaka klabu ya kuichezea baada ya kushindwa kufikia makubaliano na Bolton. (Mirror)

Mourinho amesema kuwa Luke Shaw anastahili kupewa mkataba mpya katika klabu ya Manchester United.

Arsene Wenger amesema kuwa bado ni mapema sana kwa watu kumlinganisha Aubameyang na Henry. (talkSport)

Marco Silva
Marco Silva anaweza kuteuliwa kuwa meneja wa muda wa klabu ya Chelsea kama klabu hiyo itaamua kumfukuza kazi Antonio Conte kabla ya kumalizika kwa msimu huu. (Times)

Nafasi ya Steve Walsh kama mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Everton iko shakani.

Arsenal inamtaka nyota wa klabu ya Beskitas, Oguzhan Ozyakup baada ya kumruhusu aondoke Emirates mwaka 2012.

Antonio Conte aliwaambia wachezaji wake waache kuwa na tabia za kitoto baada kurejea kutokea mapumziko ya siku tatu. (Daily Mail)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 10 Februari, 2018  Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 10 Februari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 2/10/2018 01:18:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.