Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 13 Februari, 2018

Michy Batshuayi
Borussia Dortmund itajaribu kusajili Michy Batshuayi moja kwa moja kwenye majira ya joto.

Mauricio Pellegrino hatakiwi kulaumiwa kwa matokeo mabaya ya Southampton, kwa mujibu wa kiungo wa klabu hiyo Oriol Romeu.

Leeds itarejea sokoni kusaka saini ya mshambuliaji wa klabu ya Carpi, Jerry Mbakogu kwenye majira ya joto, baada ya kushindwa kumnasa nyota huyo mwezi Januari pamoja na kupeleka ofa ya pauni milioni 3.5. (Daily Mail)

Kiungo wa Real Madrid, Dani Ceballos anaweza kuzitosa Arsenal na Liverpool na kuchagua kurejea katika klabu ya Real Betis.

Meneja wa klabu ya West Ham, David Moyes amekanusha taarifa zinazodai kuwa ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Kiungo wa klabu ya Hull City, Ray Mason ametangaza kustaafu soka baada ya kushauriwa kufanya hivyo na wataalamu wa afya kufuatia majeraha aliyopata kichwani.

Wakala wa Gareth Bale anasema kuwa thamani ya mshambuliaji huyo ni sawa na ya Neymar na haondoka Real Madrid. (talkSport)

Lionel Messi 
Timu ya taifa ya Argentuna inataka Lionel Messi achezeshwe michezo michache katika klabu ya Barcelona ili awe vizuri zaidi kwenye Kombe la Dunia 2018.

Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Alexander Lacazette atakuwa nje kwa muda wa wiki sita kufuatia majeraha aliyopata katika goti. (Sky Sports)

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho ana mpango wa kumuuza Chris Smalling na Phil Jones, huku Raphael Varane na Harry Maguire wakitarajiwa kuchukua nafasi za wawili hao.

Nahodha wa Manchester City, Vincent Kompany anasema kuwa muda umefika kwa kikosi cha Pep Guardiola kushindania taji la Ligi ya Mabingwa.

Shujaa wa klabu ya Juventus, Giorgio Chiellini amedai kuwa hakuna mbadala wa Harry Kane katika klabu ya Tottenham baada ya kumlinganisha mshambuliaji huyo na Lionel Messi. (Mirror)

Jose Mourinho ana mpango wa kuzungumza na Anthony Martial kumhakikishia kuwa bado yuko kwenye mipango yake baada ya Mfaransa huyo kupoteza nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza kwa Alexis Sanchez.

Luis Enrique anataka kuja na benchi lake la ufundi alilokuwanalo katika klabu ya Barcelona kama atachukuwa kibarua cha kuinoa Chelsea, akiwemo na meneja wa sasa wa Celta Vigo, Juan Carlos Unzue.

Josha Vagnoman
Arsenal inamfukuzia beki wa klabu ya Hamburg, Josha Vagnoman, ingawa Chelsea, Manchester City na Bayern Munich pia zimeonyesha nia ya kuaka kumsajili chipukizi huyo. (Sun)

Mkurugenzi mkuu wa Borussia Dortmund, Hans-Joachim Watzke anasema kuwa klabu yake ilitaka kuongeza kipengele cha mkataba wa kudumu katika dili la uhamisho wa mkopo wa Michy Batshuayi, lakini Roman Abramovich alilikataa ombi hilo.
 (Express)

James Tavernier yuko katika hatihati ya kusaini mkataba wa miaka mitatu na nusu katika klabu ya Rangers.

Klabu ya Barnsley inataka kufanya mazungumzo na meneja wa St Mirren, Jack Ross kuhusiana na kibarua cha kukinoa kikosi chao.

David Moyes anasema kuwa anatamani kuinoa timu ya taifa ya Uskoti siku za mbeleni, huku kukiwa na uvumi unaodai kuwa ataondoka katika klabu ya West Ham mkataba wake utakapoisha mwishoni mwa msimu huu.

Hamilton imekubali kusaini dili la uhamisho wa Kenny van der Weg na Ross Jenkins, na wawili hao wanaweza kuichezea klabu hiyo kwa mara ya kwanza dhidi Rangers siku ya Jumapili. (Record)

Mohamed Salah na Roberto Firmino wakishangilia bao
Mohamed Salah na Roberto Firmino wanaweza kuisaidia klabu ya Liverpool kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa, kwa mujibu wa kiungo wa klabu hiyo, Andy Robertson. (Star)

Aliyekuwa kiongozi katika 'Academy' ya Arsenal, Liam Brady amefichua siri ya kuwa klabu hiyo ilimwachia Harry Kane akiwa na umri wa miaka nane kwa sababu alikuwa hafanani na mwanamichezo. 

Beki wa klabu ya Aston Villa, John Terry atafanya uamuzi kuhusu hatma yake katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu. (Telegraph)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 13 Februari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 13 Februari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 2/13/2018 12:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.