Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 5 Februari, 2018

Mohamed Salah
Kwa mujibu wa Philp Babb, mshambuliaji wa Mohamed Salah ana thamani ya pauni milioni 100 kwa sasa.

Cesc Fabregas ana amini anaweza kucheza mpira kwa mingi zaidi lakini ana matamanio ya kujaribu kazi ya umeneja miaka ijayo.

Klabu ya Leeds inaweza kuteua meneja mpya ndani ya masaa 24 yajayo.

Kwa mujibu wa Cesc Fabregas, mshambuliaji wa Chelsea, Eden Hazard ana sifa zote za kutwaaa tuzo ya Ballon d'Or.

Kiungo wa klabu ya West Ham, Pedro Obiang anaweza kuukosa muda wote wa msimu huu uliosalia. (Sky Sports)

Kevin De Bruyne amesema kuwa wachezaji wa klabu ya Manchester City wanastahili kupewa mapumziko. 

Kiungo wa Real Madrid, Mateo Kovacic na golikipa wa Everton, Jordan Pickford wanatarajiwa kujiunga na klabu ya Manchester United, huku Joe Hart akitarajia kutua Chelsea kwenye majira ya joto.

Van Dijk
Virgil Van Dijk amemshutumu Harry Kane kwa kujiangusha chini katika mechi ya Liverpool dhidi ya Tottehma iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya goli 2-2. (ESPN)

Leicester imemuomba Riyad Mahrez amalize mgomo aliouanzisha mwenyewe na arejee kikosini.

Gareth McAuley anasema kuwa West Brom ilimuabisha marehemu Cyrille Regis npamoja na familia yake kwa kukubali kufungwa na Southampton. (Telegraph)

Kevin De Bruyne yuko tayari kwa mapumziko mafupi katika kipindi ambacho klabu ya Manchester City inaandamwa na majeruhi.

Rafa Benitez anafanya mpango wa kufanya mdaharo na klabu ya Newcastle juu ya mapungufu yaliyojitokeza wakati wa dirisha dogo la usaliji.

Jose Mourinho
Jose Mourinho amekanusha taarifa zinazodai ana mpango wa kusajili straika mpya kwenye majira ya joto. (Guardian)

Arsene Wenger amekiri kuwa na mawazo juu ya mstakabali wa maisha yake yajayo katika klabu ya Arsenal kama meneja.

Hector Bellerin anadai Arsenal iko tayari kuipa mshituko Ligi Kuu ya Uingereza.

Steve McClaren anaweza kuwa mmoja wa wanaowania kazi ya kuinoa klabu ya Leeds baada ya Thomas Christiansen kutimuliwa kwa kushindwa kupata ushindi mwaka 2018. (Mirror)

Gareth Southgate amesema ana hamu ya kutengeza Timu ya Taifa ya Uingereza ambayo itavutia kutazama na ambayo taifa zima litaiunga mkono. (Times)

Winga wa Leicester, Marc Albrighton amekanusha tetesi zinazodai wachezaji wa klabu hiyo wamekasirishwa na vitendo vya Riyad Mahrez. (Daily Mail)

Samuel Umtiti
Nyota wa klabu ya Barcelona, Samuel Umtiti alibaguliwa na mchezaji wa Espanyol.

Shujaa wa Uingereza, Peter Shilton anakataa mwaliko wa kukutana na Diego Maradona isipokuwa kama Mwajentina huyo ataomba msamaha juu ya goli lake la 'Mkono wa Mungu'. (Sun)

Mimi sio mpiga mbizi - mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane amemjibu beki wa klabu ya Liverpool Virgil Van Dijk.

Oliver Giroud amesema kuwa meneja wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps alimshauri aondoke Arsenal. (talkSport)

James Forrest anasisitiza kuwa Celtic inauwezo wa kutosha kuweza kukuabiliana na idadi kubwa ya majeruhi.

Jack Colback alimtuhumu Rafa Benitez kumkosea heshima baada ya kuondoka Newcastle. (Express)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 5 Februari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 5 Februari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 2/05/2018 10:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.