Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 26 Februari, 2018
Neymar na Coutinho |
Paris Saint-Germaine ina mpango wa kumnasa Philippe Coutinho kwa lengo la kumfanya Neymar aachane na uhamisho kwenda Real Madrid, kwan inaaminika kuwa Wabrazili hao wameshibana vilivyo. (El Pais)
Kiungo wa klabu ya AC Milan, Franck Kessie anasema kuwa ndoto zake ni kuja kucheza ndani ya Ligi Kuu ya Uingereza akiwa na klabu ya Manchester United.
Kevin De Bruyne anasema kuwa matamanio yake ni kutwaa mataji mengi zaidi msimu huu.
Aliyekuwa mshambulizi wa klabu ya Arsenal, Thierry Henry anasema kuwa angependa kuchukua nafasi Arsene Wenger kama meneja wa klabu hiyo.
Klabu ya Oxford United inasema kuwa Craig Bellamy yuko katika orodha fupi ya watu wanne ambao klabu hiyo inatarajia kuwateua kuchukua nafasi ya kukinoa kikosi chao.
Mshambuliaji wa Manchester United, Romelu Lukaku anasema kuwa anastahili heshima kubwa kwa rekodi yake ya kutupia nyavu. (Sky Sports)
Manchester City ina nafasi ya kushinda taji la Ligi ya Mabingwa, kwa mujibu wa Sergio Aguero.
Klabu ya Shalke 04 imempa nafasi Max Meyer, ambaye mkataba wake utaisha kwenye majira ya joto, afanye uamuzi wa kubaki au kuondoka katika klabu hiyo mapema.
Winga wa klabu ya Atletico Madrid, Nicolas Gaitan anakaribia kujiunga na Dalian Yifang inayoshiriki Ligi Kuu ya China. (ESPN)
Fernando Torres |
Fernando Torres bado anataka kubaki katika klabu ya Atletico Madrid, licha ya kuachwa nje ya kikosi kilichocheza dhidi ya Sevilla Jumapili. (Marca)
Chelsea wanaongoza mbio za kuwania saini ya Robert Lewandowski - ambaye ana matamanio makubwa ya kujiunga na Ligi Kuu ya Uingereza - ingawa klabu ya Manchester United pia inahitaji huduma ya mshambuliaji huyo.
Pep Guardiola yuko tayari kusaini mkataba mpya katika Manchester City, ambao utamfanya aitumikie klabu hiyo hadi mwaka 2021 na ataingiza karibuni pauni milioni 19.5 kwa msimu.
Mipango ya Manchester United kumsajili kiungo wa klabu ya Nice, Jean Michael Seri imeingia dosari baada ya Liverpool na Arsenal kuingilia kati.
Jurgen Klopp anamtaka kiungo wa klabu ya Bournemouth, Lewis Cook achukue nafasi ya Emre Can, ambaye anakaribia kuondoka kwenye majira ya joto, na ameandaa ofa ya pauni milioni 20.
David Brooks |
Tottenham iko kwenye mazungumzo na klabu ya ya Sheffield United juu ya uhamisho wa mshambuliaji wa klabu hiyo, David Brooks, ambaye anaaminika atakuja kuwa kama Harry Kane.
Scott Arfield anawindwa na klabu ya Vancouver Whitecaps pamoja na Montreal Impact. (Sun)
Jurgen Klopp amewaambia wachezaji wa Liverpool 'wawe na hasira' kama wanataka kumaliza Ligi katika nafasi ya juu msimu huu. (Express)
Jurgen Klopp amewaambia wachezaji wa Liverpool 'wawe na hasira' kama wanataka kumaliza Ligi katika nafasi ya juu msimu huu. (Express)
Arsene Wenger amezima tetesi zinazozungumzia hatima yake baada ya kugoma kukanusha kuwa msimu huu unaweza ukawa wa mwisho kwake, kama meneja wa klabu ya Arsenal.
Mauricio Pellegrino anaamini kwamba ari waliyo nayo wachezaji wake inaweza kuisaidia klabu hiyo iondokane na kushuka daraja msimu huu.
Joe Allen amesema kuwa hatojali kama Jack Butland ataenda kushiriki Kombe la Dunia na Timu ya Taifa ya Uingereza na amemtaka golikipa huyo kuwa makini na kiwango chake akiwa Stoke City. (Daily Mail)
Chelsea iko tayari kushindana na klabu ya Barcelona kuwania saini ya winga wa Caen, Yann Karamoh, ambaye anaichezea Inter Milan kwa mkopo.
Chelsea iko tayari kushindana na klabu ya Barcelona kuwania saini ya winga wa Caen, Yann Karamoh, ambaye anaichezea Inter Milan kwa mkopo.
Sol Campbell anaweza kuteuliwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Grimsby baada ya mwenyekiti wa klabu hiyo, John Fenty kusema kuwa yuko tayari kufanya mazungumzo na beki huyo wa Uingereza. (Mirror)
Aliyekuwa kiungo wa klabu ya Barcelona, Xavi Hernandez ameitaka Celtic itumie fedha za kutosha kama itataka kuleta upinzani barani Ulaya.
Xavi Hernandez |
Winga wa klabu ya Rangers, Daniel Candeias amesisitiza kuwa nafsi yake iko pamoja na klabu yake na sio aliyekuwa meneja wake, Pedro Caixinha, ambaye alimsajili kipindi cha nyuma. (Record)
'Kucheza soka chini ya usimamizi wa Pep Guardiola ni kama vile kuwa Chuo Kikuu,' amesema naodha wa Manchester City.
Harry Kane atalazimika kuondoka Tottenham kama ana njaa ya mataji, kwa mujibu wa Andres Villa Boas. (talkSport)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 26 Februari, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
2/26/2018 12:15:00 PM
Rating: