Loading...

Walimu na wanafunzi wakike wanusurika kutekwa na Boko Haram

Boko Haram wamekuwa wakiendesha harakati za kutaka kuwa na taifa lao la kiislamu kaskazini mwa Nigeria
Wasichana wa shule na walimu kaskazini mashariki mwa Nigeria wamefanikiwa kukimbia shambulizi lililofanywa na wanamgambo wa Boko Haram kwenye shule yao.

Walioshuhudia walisema kuwa wanamgambo hao waliokuwa na magari waliwasili kwenye mji wa Dapchi, jimbo la Yobe siku ya Jumatatu, ambapo walianza kufyatua risasi na kulipua vilipuzi.

Kusikia sauti hizo wanafunzi na walimu wao walifanikiwa kutoroka.

Soma zaidi:
Mwezi Aprili mwaka 2014, Boko Haram waliwateka nyara wasichana wa shule 270 katika mji wa kaskazini mashariki wa Chibok.

Wakaazi na raia waliojihami huko Dapchi wanasema wanaamini wanamgambo hao walikuwa na mpango wa kuwateka nyara wasichana.

Baada ya kupata shule ikiwa bila mtu wanamgambo hao waliipora.

Wanasema kuwa vikosi vya jeshi la Nigeria vikisaidiwa na ndege za jeshi, baadaye vilizima shambulizi hilo.

Mwezi Septemba mwaka uliopita zaidi ya wasichana wa shule 100 wa shule ya Chibok waliunganishwa na familia zao kwenye sherehe katika mji mkuu wa Nigeria Abuja.

Sehemu kubwa ya wasichana hao waliokolewa mwezi Mei kufuatia mpango uliokumbwa na utata wa kubadilishana wafungwa na serikali ambapo makamanda wa Boko Haram waliachiliwa.

Lakini zaidi wa wasichana 100 bado wanashikiliwa na Boko Haram na haijulikani waliko.

Wanamgambo wa Boko Haram wamekuwa wakiendesha harakati za kutaka kuwa na taifa lao la kiislamu kaskazini mwa Nigeria. Mzozo huo unaaminiwa kusababisha vifo vya maelfu ya watu.
Walimu na wanafunzi wakike wanusurika kutekwa na Boko Haram Walimu na wanafunzi wakike wanusurika kutekwa na Boko Haram Reviewed by Zero Degree on 2/20/2018 03:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.