Ombi la Somalia kujadiliwa na Wakuu wa EAC
Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki, Julius Wandera Maganda |
Maombi ya Somalia yametajwa kuwa yataingia katika majadiliano ya wakuu wa nchi hizo wanaotarajiwa kukutana kwa siku mbili kuanzia kesho jijini Kampala, Uganda.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki, Julius Wandera Maganda, suala la uwezekano wa Somalia kujiunga EAC litajadaliwa na endapo itakubaliwa, inatarajiwa kuwa mwanachama wa saba.
Na endapo itakubaliwa, basi Jumuiya ya Afrika Mashariki itakuwa na nguvu kubwa zaidi kwani itafikisha idadi ya watu milioni 190, ambao kiuchumi ni mtaji mkubwa kwa ustawi wa watu wa ukanda husika. Kuiongeza 'Pembe ya Afrika,' katika eneo la Afrika Mashariki, itaifanya jumuiya kuwa na sehemu kubwa ya pwani, katika mwambao wa Bahari ya Hindi.
Maganda ambaye ni Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Uganda, amesema pamoja na suala la Somalia, marais wa Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Sudan Kusini na Burundi watazungumzia masuala ya afya na miundombinu.
Marais, Dk John Magufuli wa Tanzania, Yoweri Museveni wa Uganda ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa EAC, Uhuru Kenyatta wa Kenyatta, Pierre Nkurunzinza wa Burundi, Paul Kagame wa Rwanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Salva Kiir watazungumzia pia masuala ya kuimarisha uchumi ndani ya jumuiya, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha magari yataanza kuundiwa ndani ya jumuiya.

Reviewed by Zero Degree
on
2/20/2018 03:44:00 PM
Rating: