Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 20 Februari, 2018

Robert Lewandowski
Mshambuliiaji wa klabu ya Bayern Munich, Robert Lewandowski amethibitisha kwamba, anatambua kuwa klabu ya Real Madrid ina nia ya kumsajili kwenye majira ya joto. (Express)

Klabu ya Real Madrid inatarajiwa kutoa ofa ya pauni milioni 100 na Gareth Bale kama sehemu ya kumnasa mshambuliaji wa Chelsea, Eden Hazard.

Sergio Agoero aingia katika mzozo na shabikiwa klabu ya Wigan baada ya Manchester City kutolewa kwenye michuano ya FA kwa kuchapwa goli 1-0.

Meneja wa Timu ya tifa ya Ubelgiji anasema kuwa siku zote Michy Batshuayi alikuwa tayri kwa klabu ya Chelsea. (talkSport)

Kiungo wa klabu ya Real Madrid, Toni Kroos ndio chaguo la kwanza la Jose Mourinho kwenye majira ya joto. (Independent)

Rakitic anahofia kuondoka kwa Andres Iniesta katika klabu ya Barcelona baada ya mambo makubwa aliyoyafanya pale.

Klabu ya Guingamp imemsajili Isaac Drogba, mtoto wa aliyekuwa mshambuliaji wa Chelsea, Didier Drogba.

Pedro Rodriguez
Pedro amesema kuwa Lionel Messi anaweza kuwa mchezaji bora wa dunia lakini haimanishi kwamba hakamatiki. (ESPN)

Wamiliki wa West Brom wamemwambia Alan Pardew arejeshe mpangilio, utulivu na matokeo mazuri katika klabu hiyo baada ya matukio ya wiki jana. (Sun)

Arsenal wamepewa matumaini na klabu ya Bordeaux kwamba, Malcom, ambaye ana thamani ya pauni milioni 40 atakuwa huru kuonodka kwenye majira ya joto.

Manuel Lanzini anategemewa kurejea katika mazoezi ya klabu ya West Ham wiki hii.

Meneja wa klabu ya Reading, Jaap Stam yuko hatari kufukuzwa kazi kama timu hiyo itapoteza mchezo dhidi ya Nottingham Forest leo usiku.

Dan Micciche anapigania kulinda kibarua chake katika klabu ya MK Dons baada ya kupoteza michezo yake mitano ya kwanza akiwa kama mkufunzi wa klabu hiyo. (Star)

Andy Carroll
West Ham ina matumaini ya kumshuhudia Andy Carroll anarejea uwanjani kabla ya msimu huu kuisha.

Klabu ya Arsenal itaongeza matumizi baada ya kufanikiwa kusaini makataba wa udhamini wenye thamani ya pauni milioni 200. (Mirror)

Wales kulipwa pauni milioni 1 kwa siku kwa kucheza katika Mashariki ya Mbali mwezi ujao - lakini ni endapo tu Gareth Bale atajumuishwa kikosini.

Wachezaji wanne wa West Bromwich Albion wanaotuhumiwa kwa wizi wa texi mjini Barcelona wanategemewa kukwepa kwenda polisi nchini Uhispania lakini watakumbana na faini ya pauni 450,000 kwa pamoja. (Daily Mail)

Alan Pardew anapigania kulinda kibarua chake katika klabu ya West Bromwich Albion wakati akijiandaa na mchezo mgumu kwenye Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Huddersfield Town wikendi ijayo. (Telegraph)

Tottenham inafanya mpango mpya wa kumnasa straika wa klabu ya Crystal Palace na Timu ya Taifa ya Ivory Coast, Wilfried Zaha kwa pauni milioni 50 kwenye majira ya joto. (Times)

Scott McTominay
Alex McLeish ana mpango wa kufanya mazungumzo na Scott McTominay wa Manchester United, lengo likiwa ni kutaka kujua kama anataka kuichezea klabu ya Scotland. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 20 Februari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 20 Februari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 2/20/2018 12:21:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.