Loading...

Watanzania 3 watakaoshiriki ndani ya semina ya FIFA


Kuelekea semina ya Shirikisho la Soka la Kimataifa ambayo itafanyika nchini Tanzania wiki hii, Watanzania watakaoshiriki ndani ya semina hiyo ni watatu.

Watanzania hao ni Rais wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Wallace Karia, Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Leodegar Tenga ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) pamoja na Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk Harrison Mwakyembe amesema hayo alipokuwa akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kwenye ukumbi wa mikutano ya Uwanja wa Uhuru.

Akizungumzia juu ya ujio huo Waziri Mwakyembe amesema mbali na semina hiyo, pia Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, John Joseph Pombe Magufuli pia anatarajiwa kukutana na kuzungumza na Rais wa Fifa, Gianni Infantino pindi atakapotua Dar, wiki hii.

“Ujumbe wa Fifa tayari unatarajiwa kuanza kuwasili leo, lakini pia Rais wa Fifa atapata nafasi ya kuzungumza na Rais Magufuli, kuhusu watazungumza nini hicho kitakuja kutajwa baadaye, pia tutawapa mwaliko rasmi wa wao kuja kututembelea.

“Kwani kwa sasa wao wanakuja kwa ajili ya semina yao, mambo mengine yatakuja baadaye,” alisema Waziri Mwakyembe.

Upande wa Kidao alisema, semina hiyo itakuwa na ajenda kadhaa, akizitaja tano ni:
  1. Soka la wanawake
  2. Soka la vijana
  3. Miradi ya taifa inayotokana na fedha za Fifa.
  4. Uendeshaji wa klabu ambapo ndani kutakuwa na masuala mbalimbali ikiwemo kuhusu leseni.
  5. Vipaumbele vya wanachama wa Caf, kuhusu kujua wanachotaka vipewe kipaumbele.
Watanzania 3 watakaoshiriki ndani ya semina ya FIFA Watanzania 3 watakaoshiriki ndani ya semina ya FIFA Reviewed by Zero Degree on 2/20/2018 04:16:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.