Loading...

Wayne Rooney aeleza anavyomchukulia Alexis Sanchez


Aliyekuwa nyota wa klabu ya Manchester United, Wayne Rooney amemtaja mchezaji mpya aliyesajiliwa na klabu hiyo, Alexis Sanchez kama mchezaji aliyekamilika, na amefananisha upatikanaji wake kama ule wa Carlos Tevez mwaka 2007.


Akizungumza na Sky Sports, Rooney amesema: “Kwangu mimi ni mchezaji aliyekamilika kwa Manchester United. Ana utayari, shauku, hamu na unaweza ukaona uwezo wake katika kufunga.”

“Ni aina ya wachezaji wanaohitajika, karibu sawa na wakati Tevez alipojiunga na Manchester United mwaka 2007”

“Anaamsha wachezaji wengine na kupata asilimia kumi ya wachezaji wa ziada wanaomzunguka. Nafikiri Alexis Sanchez atafanya hivyo.”


Rooney pia ana imani Sanchez atamsaidia Romelu Lukaku kurejea kwenye moto wake wa awali.

“Nafikiri Manchester United walikuwa wanakosa wachezaji ambao wangeweza kumsukuma Lukaku na kujaribu kumpa uhuru wa kufunga magoli mengi zaidi,” alisema Rooney.
Wayne Rooney aeleza anavyomchukulia Alexis Sanchez Wayne Rooney aeleza anavyomchukulia Alexis Sanchez Reviewed by Zero Degree on 2/07/2018 12:28:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.