Loading...

Athuman Iddy aeleza chanzo cha kuitwa 'Chuji'


KIUNGO mkabaji wa timu ya Coastal Union ya Tanga, Athuman Iddy ‘Chuji’, amesema sababu ya kuitwa jina hilo la utani la Chuji ni kutokana na kushindwa kutamka vyema neno mchuzi alipokuwa mtoto mdogo.

Chuji alisema alikuwa akitamka chuji akimaanisha mchuzi na imemfanya jina hilo limkae kuliko hata jina lake alilopewa na wazazi wake.

Alisema baba yake, Iddy Athuman aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Simba ndiye aliyechangia jina hilo kukua kwa kasi kubwa kutokana na kutembea nae sehemu nyingi, lakini moja ya sehemu waliyokuwa wanaenda sana ni kwenye migahawa ambako huko ndiko lilizidi kushamiri.

Source: Dimba
Athuman Iddy aeleza chanzo cha kuitwa 'Chuji' Athuman Iddy aeleza chanzo cha kuitwa 'Chuji' Reviewed by Zero Degree on 3/27/2018 01:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.