Loading...

Besiktas imeshtakiwa na UEFA baada ya paka kuingia uwanjani


Timu ya Besiktas imeshtikiwa na UEFA baada ya paka kuingia uwanjani wakati mchezo kati yao na Bayern Munich.

Mwamuzi wa mpira Muingereza Michael Oliver alisimamisha mechi wakati kipindi cha pili cha mchezo kwenye uwanja wa Vodafone Park hadi paka huyo alipotoka.

Mashtaka hayo yameelezwa kuwa ni "ukosefu wa mpangilio" wakati pia klabu hiyo ya Uturuki ilishitakiwa kwa "kutupa vitu uwanjani na kuziba ngazi"

Kesi hiyo itasikilizwa na bodi ya UEFA tarehe 31 Mei.

Mashabiki wa klabu hiyo ya Ujerumani walimchagua paka huyo kuwa 'mchezaji bora wa mechi'
Besiktas imeshtakiwa na UEFA baada ya paka kuingia uwanjani Besiktas imeshtakiwa na UEFA baada ya paka kuingia uwanjani Reviewed by Zero Degree on 3/16/2018 10:02:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.