Loading...

Bodi ya Manchester United yakiri 'kujutia' usajili wa Alexis Sanchez


Wanachama wa Bodi ya Manchester United wanakiri kujutia usajili wa Alexis Sanchez wakati wa mkutano wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Kwa mujibu wa Ripoti mbalimbali, wanachama wa bodi hiyo walionyesha kujutia usajili wa Alexis Sanchez wakati wa mkutano na watendaji wa ligi Kuu ya Uingereza wiki iliyopita.

Manchester United ilifanya moja kati ya usajili mkubwa katika historia ya Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kumsajili Sanchez kutoka Arsenal mwezi January.

Mkataba wa raia huyo wa Chile ulikuwa uishe mwisho wa msimu huu na mashetani wekundu wakaipiku Manchester City kwa kuipata saini yake, kwa kumpa ofa ya mshahara wa pauni laki 500,000 kwa wiki. Lakini nyota huyo wa zamani wa Arsenal na Barcelona bado hajafanikiwa kuonyesha uwezo wake katika dimba la Old Trafford.

Sanchez alitoa 'assist' mbili wakati Manchester United ilipocheza dhidi ya Yeovil kwenye FA Cup. Lakini ndani ya michezo sita ya United amefunga goli moja pekee la penalti dhidi ya Huddersfield. Ripoti nyingi zimeibuka na kudai kwamba wamachama wa bodi Old Trafford wanajutia kumsajili mshambuliaji huyo.

Mshahara wake pia umesababisha mvutano ndani ya chumba cha kubadilishia nguo, ambapo raia huyo wa Chile analipwa zaidi ya mara mbili ya baadhi ya wachezaji wenzake wa Manchester United.

Mashetani wekundu wanatarajiwa kuendeleza matumizi yao kwenye usajili wa majira ya joto, huku kukiwa na majina kadhaa yaliyotajwa kuwa mstari wa mbele kwenye orodha ya Jose Mourinho.
Bodi ya Manchester United yakiri 'kujutia' usajili wa Alexis Sanchez Bodi ya Manchester United yakiri 'kujutia' usajili wa Alexis Sanchez Reviewed by Zero Degree on 3/05/2018 09:13:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.