Loading...

Chelsea, Real Madrid zinatarajiwa kubadilishana wachezaji hawa


Chelsea imeripotiwa kuwa kwenye mchakato wa kutaka kumshawishi Asensio atue Stamford Bridge kutoka Real Madrid.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, chanzo kimoja kutoka Chelsea kimesema kuwa nyota huyo wa Real Madrid, Marco Asensio atavaa jezi ya Eden Hazard.

Antonio Conte hatarajiwi kuhusika na kibarua cha kuijenga upya klabu ya Chelsea, huku aliyekuwa mkufunzi wa Barcelona, Luis Enrique akitarajiwa kuchukuwa nafasi yake Stamford Bridge msimu ujao.

Marco Asensio
Nafasi ya Asensio kwenye kikosi cha kwanza Real Madrid msimu huu imekuwa ni ya mshaka, ambapo alipata muda wa kutosha mwanzoni mwa msimu lakini tangu kumetokea mabadiliko kwenye mfumo wa upangaji wa kikosi anaoutumia Zinedine Zidane amekuwa akiachwa benchi na tayari kuna ripoti ambazo zinadai nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 atakuwa anavaa jezi namba 10 katika klabu ya Chelsea msimu ujao.

Eden Hazard
Real Madrid wanataka kumsajili Eden Hazard, ambaye anayevaa jezi namba 10 katika klabu ya Chelsea. Nyota huyo anaweza kutumika kwenye dili la uhamisho utakaoambatana na kubadilishana wachezaji. Hata hivyo, Asensio anatambua kuwa anaweza kulazimisha uhamisho wake kuondoka Bernabeu kama vigogo hao wa La Liga watakataa kumuuza.
Chelsea, Real Madrid zinatarajiwa kubadilishana wachezaji hawa Chelsea, Real Madrid zinatarajiwa kubadilishana wachezaji hawa Reviewed by Zero Degree on 3/19/2018 02:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.