Jamhuri yapinga dhamana ya Viongozi Chadema, kesi yaanza tena
Katika uamuzi huo Hakimu mkazi mkuu, Wilbard Mashauri alisema washtakiwa wanatakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini hati ya dhamana ya Sh milioni 20, kuwa na barua kutoka kwa viongozi wao wa vijiji au mtaa na kuwa, nakala za vitambulisho vyao na kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam kila Alhamisi kisha kusema asiyeridhika na uamuzi huo ana haki ya kukata rufaa.
Upande wa Jamhuri umewasilisha notice mahakamani kupinga dhamana hiyo ambapo kesi inaendelea ten jioni hii, huku kukiwa na kuna mvutano mkubwa wa kisheria ambapo kwa sasa upande wa uetetezi unawasilisha hoja zao mbele ya hakimu.
Wakili wa viongozi wa Chadema, Peter Kibatala ameipinga taarifa ya rufaa iliyotolewa na wakili wa Serikali akiiomba mahakama itekeleze amri yake ya dhamana kwa kuwasainisha washtakiwa bondi ya Sh20 milioni katika tarehe ambayo inaona inafaa, baada ya hapo ndiyo ipokee taarifa hiyo ya Serikali ya kukata rufaa.
Kwa upande wake, Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi amedai kuwa suala hilo hilo la kisheria kwani taarifa ya rufaa ikishawasilishwa mahakamani na kupokelewa, mahakama haiwezi kuongea chochote juu ya taarifa hiyo, hivyo itakuwa imeingia katika kumbukumbu za mahakama.
Kwa upande wake, Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi amedai kuwa suala hilo hilo la kisheria kwani taarifa ya rufaa ikishawasilishwa mahakamani na kupokelewa, mahakama haiwezi kuongea chochote juu ya taarifa hiyo, hivyo itakuwa imeingia katika kumbukumbu za mahakama.
Jamhuri yapinga dhamana ya Viongozi Chadema, kesi yaanza tena
Reviewed by Zero Degree
on
3/29/2018 04:15:00 PM
Rating: