Loading...

Kesi inayowakabili Aveva, Kaburu kuanza kusikilizwa mwezi ujao


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), imeieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa imeshakamilisha upelezi wa kesi ya Rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange 'Kaburu' na wapo tayari kuanza kusikilizwa.

Aveva leo ameshindwa kuhudhuria tena mahakamani katika kesi yake utakatishaji fedha inayomkabili ikiwa ni mara ya saba mfululizo kutokana kutokana na kulazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufuatia hali yake ya kiafya kutokuwa nzuri.

Aveva anakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha kiasi cha dola 300,000 za Kimarekani akiwa na makamu wake wa rais Geofrey Nyange 'Kaburu'.

Katika kesi hiyo ambayo itakuwa ikisikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Makahama ya Kisutu, Thomas Simba badala ya Victoria Nongwa ambapo wakili wa Takukuru, Nassor Katuga ameiambia mahakama hiyo kwamba kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini wameshakamilisha upepelezi hivyo wapotayari kuendelea kwa hatua ya kuanza kusikilizwa.

Katuga alisema kuwa kusema kuwa lakini wapokea taarifa kuwa mshitakiwa namba moja (Aveva) ameshindwa kufika mahakamani kwa kuwa anaumwa na melazwa Muhimbili nabadala yake yupo Kaburu peke yake ambaye ni mshitakiwa namba mbili.

Kwa upande wa hakimu Simba alisema kuwa ni vyema kufuatilia hali yake kwa kuwa kesi ipo tayari kusilizwa ili iweze kuendana na muda kutona na kuwa ni ya muda mrefu ambapo amepanga kuanza kusilizwa Aprili 5, mwaka huu.
Kesi inayowakabili Aveva, Kaburu kuanza kusikilizwa mwezi ujao Kesi inayowakabili Aveva, Kaburu kuanza kusikilizwa mwezi ujao Reviewed by Zero Degree on 3/22/2018 04:18:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.