Loading...

Kesi ya Nabii Tito yapigwa kalenda


KESI ya kujaribu kujiua kwa kujichana tumbo na wembe inayomkabili mshtakiwa Onesmo Machibya maarufu Nabii Tito, imeahirishwa katika Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma hadi Machi 19, 2018.

Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, James Karayemaha aliagiza mtuhumiwa huyo kuchukuliwa vipimo vya akili katika Taasisi ya Magonjwa ya Akili ya Isanga, Dodoma ili kubaini iwapo ana matatizo hayo.
Mtuhumiwa huyo (Nabii Tito) hakufika mahakamani leo ambapo kesi yake iliahirishwa na Hakimu wa Mahakama hiyo, Mwajuma Lukindo baada ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo, James Karayemaha kutokuwepo mahakamani.
Nabii Tito alifikishwa kortini kwa mara ya kwanza Januari 29, 2018 na kusomewa mashtaka ya kujaribu kujiua kwa kujikata na wemb ambapo anadaiwa kufanya tukio hilo Januari 25, 2018 wakati akiwa mahabusu.
Kesi ya Nabii Tito yapigwa kalenda Kesi ya Nabii Tito yapigwa kalenda Reviewed by Zero Degree on 3/05/2018 06:33:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.