Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 5 Machi, 2018

Thierry Henry
Thierry Henry amesema kuwa yuko tayari kuchukua nafasi ya Arsene Wenger kama meneja wa klabu ya Arsenal endapo atahitajika.

Kwa mujibu wa Toni Cascarino, mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Eden Hazard atalazimisha kuondoka Stamford Bridge kama Conte atabaki. (talkSport)

Alan Pardew ataendelea kuwa meneja wa klabu ya West Brom kwa mechi ya wikendi ijayo dhidi ya Leicester City.

Barcelona iko hatari kumkosa Andres Iniesta kwenye mechi yao ya Ligi ya Mabingwa katika raundi ya 16 bora dhidi ya Chelsea baada ya kiungo huyo kuumia.

Klabu ya Birmingham imemtanga Garry Monk kuwa kama meneja mpya wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu.

Jack Wilshere aomba msamaha kwa msahabiki wa Arsenal baada ya timu yao kufungwa mechi nne mfululizo. (Sky Sports)

Everton inatarajia kumoa Arsene Wenger ofa ya kurejea Ligi Kuu ya Uingereza kama atafukuzwa kazi na Arsenal.

Anthony Martial anadai kwamba Paul Pogba ni 'kiungo bora dunia' na kutabili kuwa mchezaji mwenzake wa Manchester Uinted atatwaa taji ya Ballon d'Or miaka mitano ijayo. (Star)

Bayer Minich ina mpango wa kumsajili beki wa klabu ya Independiente, Fabricio Bustos kwenye majira ya joto.

Golikipa wa klabu ya Koln, Timo Horn amewaomba msamaha mashabiki wa klabu hiyo baada ya makosa yake kuigharimu timu yake kuchapwa goli 3-2 dhidi ya Sturttgart.

Joshua Kimmich
Joshua Kimmich anakaribia kusaini mkataba mpya na klabu ya Bayern Munich, ambao utamfanya aitumikie klabu hiyo hadi mwaka 2023. (Kicker)

Arsenal walituma skauti wao akamchunguze nyota anayewindwa na Manchester United anayeichezea klabu ya Benfica, Andrija Zivkovic wakati wa mechi yao dhidi ya Maritimo. 
(Sun)

Lionel Messi alifunga goli lake la 600 wakati Barcelona ilipoibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Atletico Madrid. (Marca)

Kiungo wa West Brom, Chris Brunt anakiri kuwa wachezaji wa klabu hiyo hawajacheza kwa bidii msimu huu na kwamba lawama zote asitupiwe meneja wa klabu hiyo, Alan Pardew.

Sam Allardyce anakiri kwamba klabu ya Everton inaendelea kuporomoka, huku akipigana kulinda kibarua chake. (Express)

Florian Thauvin
Aliyekuwa meneja wa timu ya taifa ya Ufaransa, Raymond Domenech ana amini kuwa Florian Thauvin anatakiwa ajumuishwe katika kikosi cha Didier Deschamps kwenye Kombe la Dunia mwaka 2018 mbele ya Ousmane Dembele na Kingsley Coman. (L'Epuipe)

Baada ya kuchapwa na klabu ya Brighton, Arsene Wenger amekiri kuwa Arsenal haiwezi kumaliza Ligi Kuu katika nafasi katika nne bora.

Meneja wa klabu ya Stoke City, Paul Lambert anataka kumsajili moja kwa moja beki wa Chelsea, Kurt Zouma ambaye anaichezea klabu hiyo kwa mkopo.

Winga wa klabu ya Stoke City Bojan - ambaye anichezea Alaves kwa mkopo - anawindwa na Bologna ya Italia.

Brighton itampa Ben White ofa ya mkataba mpywa wenye maslahi mazuri kumfanya aachane na mawazo ya ofa kutoka vilabu vikubwa vya Ligi Kuu ya Uingereza.
 (Mirror)

Pep Guardiola anasema kuwa jambo la msingi kwa Manchester City muda huu ni kuwa Mabingwa, na kwamba hayuko anafukuzia rekodi. (Independent)

Ryan Sessegnon anatarajiwa kutua Manchester City akitokea klabu ya Fulham wakati Jean Michael Seri akitarajiwa kutua Liverpool akitokea Nice.

David Alaba 
Beki wa Bayern Munich, David Alaba anatazamia kuondoka katika klabu hiyo, huku Barcelona na Real Madrid zikiwa na nia ya kumsajili nyota huyo kutoka Austria. (ESPN)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 5 Machi, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 5 Machi, 2018 Reviewed by Zero Degree on 3/05/2018 06:24:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.