Loading...

Ombi la Boniface Mkwasa kwa mashabiki wa Yanga

Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa
Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amewaondoa hofu mashabiki wa Yanga akiwataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanjani kesho.

Mkwasa alisema shabiki ni mchezaji wa 12, hivyo kujitokeza kwa wingi kutaongeza kutoa hamasa kwa wachezaji kupambana.

Aliongeza kuwa, kikosi chao kipo fiti kwa ajili ya mchezo huo, amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi.

Yanga itakabiliana na Township Rollers ya Botswana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika katika uwanja wa taifa, Dar es Salaam, saa 10 kamili jioni.
Ombi la Boniface Mkwasa kwa mashabiki wa Yanga Ombi la Boniface Mkwasa kwa mashabiki wa Yanga Reviewed by Zero Degree on 3/05/2018 04:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.