Loading...

Kiungo wa Real Madrid anayeitamani Liverpool


Dani Ceballos 'anatarajia kushinikiza uhamisho wake kwenda klabu ya Liverpool' ya Ligi Kuu ya Uingereza.

Kulingana na ripoti zilizotolewa nchini Uhispania, mchezaji huyo alionyesha mtamanio ya kuondoka Bernabeu wakati alipokuwa akizungumza na rais wa Real Madrid, Florentino Perez.

Hamu ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kuondoka Bernabeu kwenye majira ya joto inazidi kuongezeka, akiwa meonekana kwenye mechi 19 pekee za vigogo hao msimu huu. Liverpool ni miongoni mwa iklabu zinazofuatilia hali ya Ceballos na ina matumaini ya kufanikisha dili la kumleta EPL.

Dani Ceballos
Mchezaji huyo anaripotiwa kuwa na hamu ya kujaza nafasi iliyoachwa na Philippe Coutinho, ambaye alijiunga na Barcelona kwenye usajili wa mwezi Januari na, kulingana na taarifa za Uhispania, Ceballos amefanya mazungumzo zaidi na rais Perez juu ya uhamisho wake kwenye majira ya joto.

Liverpool wanaamini kuwa wanaweza kumnasa kiungo huyo kwa pauni milioni 30 tu wakati wa majira ya joto na wana matumaini kwamba hamu ya Ceballos kutua Anfield inaweza kuthibitika kuwa imara.
Kiungo wa Real Madrid anayeitamani Liverpool Kiungo wa Real Madrid anayeitamani Liverpool Reviewed by Zero Degree on 3/22/2018 02:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.