Kocha PSG ataja tarehe ya Neymar kurejea uwanjani
Neymar, ambaye anategemewa na kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kwenye Kombe la Dunia litakaloanza tarehe 14 Juni nchini Urusi, alipata majeraha ya mguu mwezi Februari tarehe 25 wakati timu yake ikicheza dhidi ya Marseille na kurudi Brazil kwa matibabu.
Aliukosa mchezo wao wa marudiano dhidi ya Real Madrid uliochezwa Machi 6 na kumalizika kwa PSG kutolewa nje ya Ligi ya Mabingwa.
Ile "miezi miwili na nusu hadi mitatu" ya awali ingemanisha ndio mwisho wa msimu wa Neymar katika klabu ya PSG. Lakini kwa mshambuliaji, aliyeumia wakati wa Kombe la Dunia 2014 na kuukosa mchezo wa nusu fainali dhidi ya Ujerumani uliomalizika kwa Brazil kuchapwa goli 7-1, lengo lilikuwa kujiweka sawa kwa ajili ya michuano ya mwaka huu.
Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi alienda kumjulia hali Neymar nchini Brazil mwezi Machi katikati, ikiwa ni sehemu ya kuzima uvumi uliodai nyota huyo angeweza kuondoka Paris mwaka mmoja baada ya kuwasili kwake.
"Madaktari hawajafikia hatua ya kutaja siku husika ambayo atarejea," Al-Khelaifi alisema wakati ule.
Neymar na meneja wa PSG, Unai Emery |
Hata hivyo, meneja wa PSG, Unai Emery amesema nyota huyo anatarajiwa kurejea ndani ya wiki mbili hadi tatu zijazo, ikiwa na maana kwamba kuanzia tarehe 13 hadi 21 mwezi Aprili, Neymar atakuwa fit.
Kocha PSG ataja tarehe ya Neymar kurejea uwanjani
Reviewed by Zero Degree
on
3/31/2018 08:31:00 AM
Rating: