Loading...

CUF yampiga 'STOP' Maalim Seif


CHAMA cha Wananchi (CUF) mkoani Mwanza kimempiga marufuku Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad kutofanya mikutano na vikao vya kisiasa katika wilaya za Nyamagana na Ilemela zilizoko jijini hapa.

Hatua hiyo ya kumpiga marufuku Maalim Seif aliyesimamishwa uongozi na Baraza Kuu la Uongozi la CUF Taifa, imetolewa juzi katika tamko la pamoja la viongozi katika wilaya za Ilemela za Nyamagana mkoani Mwanza.

Viongozi hao waliongozwa na Mwenyeviti wa CUF wa Wilaya ya Nyamagana, Salum Mkumbukwa aliyekuwa ameambatana na wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa, Martha Haule na Zainabu Ally.

Walidai kuwa wamesikia kuwa Maalim Seif anawasili jijini Mwanza kwa siri kupitia mwavuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwa lengo la kuhudhuria kongamano moja la chama cha siasa linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni katika wilaya za Nyamagana na Ilemela akiwa na lengo la kukutana na wanachama wa CUF, jambo ambalo uongozi halina tija kwa wakati huu wakati akiwa amesimamishwa uongozi. Viongozi hao walisema wamemwandikia barua Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na wakuu wa wilaya za Nyamagana na Ilemela kupinga ujio wake.

Katika barua hiyo ambayo gazeti hili limepata nakala yake, viongozi hao wamekidai kuwa ujio wa Maalim Seif jijini Mwanza ni batili kwa madai kuwa uongozi wa Taifa hautambui kama kiongozi kwa madai kuwa alishasimamishwa uongozi na Baraza Kuu la CUF tangu mwaka jana.

Maalim Seif anatuhumiwa na wanachama wa CUF Mkoa wa Mwanza kwa jaribio lake la kutaka kumzuia Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba kuendelea kuwa kiongozi wao.

Pia anatuhumiwa kuhujumu ukuaji wa chama hicho kisiasa kwa kuanzisha migogoro na kuwagawa wanachama katika makundi jambo ni kinyume cha Katiba ya CUF.
CUF yampiga 'STOP' Maalim Seif CUF yampiga 'STOP' Maalim Seif Reviewed by Zero Degree on 3/31/2018 10:15:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.