Loading...

Manchester United kuambulia patupu kwa mshambuliaji huyu

Anderson Talisca
Hivi karibuni Manchester United imekuwa ikihusishwa na uhamisho wa straika wa Brazil, Anderson Talisca na ripoti nyingi kudai kwamba atasajiliwa kwa ada ya pauni milioni 35 kutoka Benfica kwenye majira ya joto. Lakini inaonekana juhudi za United zimegonga mwamba baada ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 kusaini mkataba mpya na Besiktas.

Talisca alijiunga na klabu ya Besiktas akitokea Benfica kwa mkopo kwenye majira ya joto 2017 na kusaini mkataba wa mwaka mmoja, huku kukiwa na kipengele cha klabu hiyo kuweza kumnunua moja kwa moja. Kulingana na taarifa zilizotoka, Besiktas inapanga kutimiza kipengele cha mkataba wao na kulipa kiasi pauni milioni 18 kwa klabu hiyo ya Ureno na kumnasa nyota huyo moja kwa moja.

Taarifa iliyotewa na Gazeti la A Bola nchini Ureno inadai kwamba Anderson Talisca anaweza kusajiliwa na Besiktas kwa lengo la kuongeza thamani yake na kumuuza kwa faida siku za mbeleni.

Hili ni pigo kubwa kwa Manchester United, ambayo si tu italazimika kulipia kiasi kikubwa cha fedha kumpata Talisca lakini inaweza kumpoteza pia kwa vilabu vingine kama vile Wolves na Liverpool ambazo zimekuwa zikimfuatilia nyota huyo kwa karibu.

Talisca ameifungia Besiktas magoli 16 katika msimu huu wa 2017/18.
Manchester United kuambulia patupu kwa mshambuliaji huyu Manchester United kuambulia patupu kwa mshambuliaji huyu Reviewed by Zero Degree on 3/23/2018 03:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.