Loading...

Manchester United wanampango wa kusajili mchezaji mwingine kutoka Arsenal


Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, Manchester United wanatazamia kumsajili beki wa klabu ya Arsenal, Hector Bellerin.

Beki huyo kutoka Arsenal alisaini mkataba wa miaka sita mwezi Octoba 2016, lakini alijaribu kufanya mipango ya kurejea Barcelona kwenye majira ya joto mwaka jana.

Mapema mwezi huu, kuna ripoti zilitolewa zikidai kuwa raia huyo wa Uhispania ataondoka Arsenal mwishoni mwa msimu huu, baada ya kuona mabadiliko ya kiwango cha Alex Oxlade-Chamberlain tangu aondoke katika klabu hiyo kwenda Liverpool.

Hector Bellerin
Inadaiwa kwamba Arsenal wako tayari kumwachia aondoke kwa ada ya pauni milioni 50 kwa lengo la kufanikisha mipango yao ya usajili wa wachezaji wapya kwenye majira ya joto.

Tovuti ya 'The Manchester Evening News' imetoa ripoti inayodai kwamba United tayari wameshafanya mawasiliano na upande wa Bellerin na kuomba kupewa taarifa muhimu ikiwa kama kutakuwa na lolote linaendelea kuhusu uhamisho wa nyota huyo. Na kama kweli wataingia kwenye mbio hizo, basi Manchester United watakabiliana na ushindani kutoka Barcelona na Juventus.
Manchester United wanampango wa kusajili mchezaji mwingine kutoka Arsenal Manchester United wanampango wa kusajili mchezaji mwingine kutoka Arsenal Reviewed by Zero Degree on 3/15/2018 04:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.