Loading...

Msuva atwaa tuzo ya mchezaji bora Morocco


KLABU ya Difaa El Jadida ya nchini Morocco anayoichezea Mtanzania, Simon Msuva, imemtangaza mchezaji huyo kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari, mwaka huu.

Hiyo imekuja siku chache tangu winga huyo apige ‘hat trick’ kwenye ushindi wa mabao 10-0 wakati timu hiyo ilipocheza na Benfica ya Guinea Bissau katika mchezo wa raun­di ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Msuva alifunga ma­bao hayo katika dakika za 44, 72 na 88 na ku­fanikisha kufikisha ‘hat trick’ hiyo kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na timu hiyo.

Msuva alijiunga na timu hiyo kwenye msimu huu wa Ligi Kuu ya Morocco akitokea Yanga baada ya klabu hiyo kuuvunja mkataba.

Difaa ilimtangaza win­ga huyo juzi Jumatatu kuwa mchezaji bora kutokana na kiwango kikubwa anachokionye­sha ndani ya uwanja ikiwemo kufunga na kutengeneza mabao.

Akizungumza na Championi Jumatano, Msuva alisema: “Kwanza ka­bisa niwashukuru Watanzania kwa kuniombea nifanye vizuri tangu nifike huku na huu ni mwanzo wangu, ninaamini kadiri siku zinavyokwen­da nitaendelea kufanya vizuri zaidi.

“Nimepanga kuipepe­rusha vema bendera ya Tanzania kwa kuifanyia mengi mazuri ikiwemo hili la mimi kuchaguliwa kuwa mchezaji bora, ninafahamu bado nina safari ndefu ya mafani­kio.”
Msuva atwaa tuzo ya mchezaji bora Morocco Msuva atwaa tuzo ya mchezaji bora Morocco Reviewed by Zero Degree on 3/07/2018 04:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.