Loading...

Dembele atakuwa tayari kujiunga na klabu ya Arsenal kwa sharti moja


Winga wa klabu ya Barcelona na Timu ya Taifa ya Ufaransa, Ousmane Dembele anaweza kushawishika kwenda Arsenal kwenye majira ya joto.

Nyota huyo aliyesajiliwa na klabu ya Barcelona kutoka Borussia Dortimund kwa kiasi kikubwa cha pesa amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi kwenye kikosi cha Ernesto Valverde. Dembele amekaa nje baada ya kupata majeraha mapema msimu huu.

Hata hivyo, hata badaa ya kupona majeraha yake vizuri, kiungo huyo bado sio chaguo la kwanza la Valverde kumchezesha na Lionel Messi pamoja na Luis Suarez kwenye safu ya ushambuliaji ya Barcelona. 

Kwa mujibu wa ripoti za nchini humo (Uhspania), Dembele amekosa raha kabisa ya kuwa Nou Camp chini ya Valverde.

Ripoti hizo zinatambua kwamba, Arsenal ina matamanio makubwa ya kumnasa Mfaransa huyo kwenye majira ya joto aje kucheza na aliyekuwa mchezaji mwenzake wa Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang.

Ousmane Dembele anaweza kuamua kujiunga na klabu ya Arsenal endapo Barcelona itamsajili Antoine Griezmann kwenye majira ya joto, dili ambalo litamfanya winga huyo aendelee kusubiri zaidi kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza Nou Camp.

Dembele ameanza na kikosi cha kwanza kwenye mechi nne pekee katika michuano yote akiwa Barcleona hadi sasa, na kutoa 'assist' mbili.
Dembele atakuwa tayari kujiunga na klabu ya Arsenal kwa sharti moja Dembele atakuwa tayari kujiunga na klabu ya Arsenal kwa sharti moja Reviewed by Zero Degree on 3/07/2018 05:07:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.