Mwigulu ataka viboko vitumike inapobidi
Akizungumza katika harambee ya ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari Lulumba Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Dk Nchemba amesema walimu wanatumia fimbo kunyoosha nidhamu za wanafunzi ili kutengeneza hatma ya nchi.
Amesisitiza kuwa ni lazima kuendelea kulinda hadhi za walimu kwa kuwapatia miundombinu bora ya ofisi na vyumba vya madarasa.
Mbali na hayo Dk. Nchemba ameongeza kwamba majengo ya taasisi yanapaswa kuwa bora zaidi na sio kutumia ramani za awali pekee kwani zinapaswa kuboreshwa kulingana na maendeleo yaliyopo.
"Kuna wakati walimu wananyoosha nidhamu za wanafunzi lakini kuna watu wengine hawaoni haya ila wao ni kulalamika tu, kinachofanyika ni kwa manufaa yetu. Niwaombe kwenye kutumia mifano tumieni mifano na kwenye kutumia fimbo fanyeni hivyo ili kutengeneza taswira ya nchi yetu," amesema Dk Mwigulu.
Amesisitiza kuwa ni lazima kuendelea kulinda hadhi za walimu kwa kuwapatia miundombinu bora ya ofisi na vyumba vya madarasa.
Mbali na hayo Dk. Nchemba ameongeza kwamba majengo ya taasisi yanapaswa kuwa bora zaidi na sio kutumia ramani za awali pekee kwani zinapaswa kuboreshwa kulingana na maendeleo yaliyopo.
"Naunga mkono ujenzi huu wa mabweni ya wanafunzi, ukarabati wa vyumba vya madarasa na ofisi za walimu hivyo nachangia mifuko 200 ya saruji nawaahidi pia kutoa Sh milioni sita," alieleza.
Mwigulu ataka viboko vitumike inapobidi
Reviewed by Zero Degree
on
3/24/2018 12:25:00 PM
Rating: