Loading...

Okwi aibuka mchezaji bora wa Simba


MSHAMBULIAJI Mganda wa Simba, Emmanuel Okwi amefanikiwa kuibuka mchezaji bora wa mwezi Januari- Februari kwa Klabu ya Simba baada ya jana Alhamisi kutangazwa rasmi.

Okwi tayari mwanzoni mwa msimu huu alifanikiwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara wa mwezi Agosti na mpaka sasa amefanikiwa kufunga mabao 16 kwenye ligi.

Hata hivyo, Mganda huyo alipata nafasi hiyo baada ya mashabiki wa soka kupewa fursa ya kuwapigia kura wachezaji wa Simba, alifanikiwa kupata kura nyingi zaidi.

Okwi alitangazwa rasmi siku ya jana na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, George Masatu kuwa ndiye mchezaji bora wa mwezi Januari-Februari kupitia mtandao wa Simba maarufu kama Simba App.

Hata hivyo mwezi Desemba mchezaji ambaye aliibuka kuwa mchezaji bora wa mwezi wa klabu hiyo alikuwa ni kipa Aishi Manula ambaye alikuwa amecheza michezo sita mfululizo bila kuruhusu bao lolote.
Okwi aibuka mchezaji bora wa Simba Okwi aibuka mchezaji bora wa Simba Reviewed by Zero Degree on 3/02/2018 09:59:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.