Loading...

Rais wa klabu hii ana mpango wa kumsajili Cristiano Ronaldo

Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid na Timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo
Rais wa klabu ya Besiktas, Fikret Orman ana mipango mikubwa kwa vigogo hawo wa Uturuki, ikiwa ni pamoja na kuja kumsajili Cristiano Ronaldo huko mbeleni.

Orman anadai Besiktas ina historia ya kuwa na utajiri mkubwa na iko miongoni mwa klabu zenye uwezo mkubwa wa kifedha. Hata hivyo, alikubali kwamba kiwango cha klabu hiyo kwa sasa sio kizuri.

Orman alisema: “Kwa sasa Besiktas haiko kwenye kiwango ambacho tunahitaji, tuna kazi kubwa ya kufanya kurejea kwenye hali yetu ya kawaida.

“Tumefika kiwango ambacho klabu yetu haistahili. Besiktas ni klabu ambayo iko kwenye viwango vya kimataifa na uzoefu wa miaka 115. Katika hatua hii, hatuko sawa ipasavyo, lakini tutafanya vizuri. Hatutakiwi kuwa hapa tulipo, tunahitaji muda na kufanya kazi. Tuna kazi kubwa ya kufanya kwa Ronaldo.”

Hivi karibuni Ronaldo amekuwa akihusishwa na klabu hiyo ya Utururki. Kulikuwa na taarifa zilizodai kwamba nyota huyo atakuwa tayari kujiunga na klabu ya Besiktas, ambayo imefanikiwa kuwashawishi Wareno wenzake kama Pepe na Ricardo Quaresma kujiunga nao, lakini inaonekana uhamisho huo unaweza usifanikiwe katika siku za hivi karibuni kwani Ronaldo bado yuko kwenye kiwango cha juu.
Rais wa klabu hii ana mpango wa kumsajili Cristiano Ronaldo Rais wa klabu hii ana mpango wa kumsajili Cristiano Ronaldo Reviewed by Zero Degree on 3/18/2018 03:31:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.