Loading...

Ripoti: Vijana 90 huambukizwa virusi vya UKIMWI ndani ya masaa 24 Tanzania


Kwa mujibu wa ripoti ya tathmini ya mazingira ya kisheria katika mwitikio wa Ukimwi iliyozinduliwa Desemba 01, 2018 katika kilele cha siku ya Ukimwi Duniani. Vijana 72 wa kike na 18 wa kiume wenye umri kati ya miaka 14 na 24 wanapata maambukizo mapya ya virusi vya Ukimwi (VVU) kila siku.

Akielezea tathmini ya ripoti hiyo leo Jumatatu Machi 12,2018 na wadau wa masuala ya Ukimwi mjini Dodoma, Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kuthibiti Ukimwi (Tacaids), Dkt. Leonard Maboko amesema tathmini hiyo ilibaini watu 81,000 nchini wanapata maambukizo mapya kwa mwaka ambayo ni sawa na wastani wa watu 225 kwa siku.

Dkt. Maboko amesema tathmini imeonyesha kati ya watu 225 wanaoambukizwa VVU kwa siku asilimia 40 ambayo ni sawa na watu 90 ni vijana kati ya miaka 14-24. Na kwenye vijana hao 90 wasichana 72 huambukizwa kwa siku huku wavulana 18 pekee ndio huambukizwa VVU.

Tathmini ya ripoti hiyo ilifanyika katika mikoa 11 ambayo ni Tabora, Katavi, Shinyanga, Mara, Dar es Salaam, Pwani, Mbeya, Rukwa, Njombe, Iringa na Ruvuma wakati kwa Zanzibar ilifanyika Unguja na Pemba.

Source: Mwananchi
Ripoti: Vijana 90 huambukizwa virusi vya UKIMWI ndani ya masaa 24 Tanzania Ripoti: Vijana 90 huambukizwa virusi vya UKIMWI ndani ya masaa 24 Tanzania Reviewed by Zero Degree on 3/12/2018 02:21:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.