Loading...

Liverpool, Manchester United kutoana jasho kwa nyota huyu wa Barcelona


Liverpool na Manchester United zinawania saini ya kiungo wa timu ya taifa ya Croatia.

Kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa nchini Uingereza na Uhispania, Liverpool FC imejiunga na Manchester United kwenye mbio za kuwania saini ya Ivan Rakitic kutoka FC Barcelona.

Taarifa hizo zinadai Liverpool wako tayari kukabiliana na Mashetani wekundu katika kuwania kumnasa nyota kutoka FC Barcleona.

Ivan Rakitic
Kwa mujibu wa taarifa kama hiyo, Rakitic amekuwa katia rada za meneja wa Manchester United, Jose Mourinho, yote ikiwa ni mapango ya kutaka kuboresha safu yake ya kiungo. Hata hivyo, taarifa hiyo inadai kuwa klabu ya Liverpool pia imeonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo huyo wa Barcelona kwenye majira ya joto.

Liverpool wantarajiwa kuingia sokoni kusaka viungo kwenye majira ya joto baada ya kumuuza Philippe Coutinho kwenda FC Barcelona mwezi Januari na pia wanaweza kumpoteza Emre Can kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu.
Liverpool, Manchester United kutoana jasho kwa nyota huyu wa Barcelona Liverpool, Manchester United kutoana jasho kwa nyota huyu wa Barcelona Reviewed by Zero Degree on 3/12/2018 04:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.