Ripoti ya CAG yabaini ufisadi CWT na NIDA
Akizungumza wakati wa kukabidhi matokeo ya ripoti ya ukaguzi maalumu kwa Rais John Magufuli leo jijini Dar es Salaam, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG Profesa Mussa Assad amesema ukaguzi wa NIDA ulibainisha ubadhilifu mkubwa wa fedha uliotokana na uzembe katika ukodishaji wa ofisi za mamlaka hiyo.
Pro. Assad ameeleza kuwa, ukodishaji wa eneo la ofisi za NIDA ulionekana ni mita za mraba 2,200 lakini wakati wa ukaguzi walipopima ilibainika eneo halisi ni mita za mraba 1,945 na kwamba kulikuwa na mita za mraba hewa 254 zenye thamani ya kiasi cha milioni 402.
Kuhusu ukaguzi wa CWT, Prof. Assad amesema ukaguzi ulibainisha uwepo wa mapungufu katika uendeshaji wa taasisi hiyo, ambapo kulikuwa na ukiukwaji wa kanuni za fedha ikiwemo utolewaji wa malipo ya fedha bila ya kuidhinishwa na Katibu Mkuu au Mweka hazina wa CWT.
Pro. Assad ameeleza kuwa, ukodishaji wa eneo la ofisi za NIDA ulionekana ni mita za mraba 2,200 lakini wakati wa ukaguzi walipopima ilibainika eneo halisi ni mita za mraba 1,945 na kwamba kulikuwa na mita za mraba hewa 254 zenye thamani ya kiasi cha milioni 402.
“Ukaguzi maalumu wa chama cha walimu Tanzania, tukatoa matokeo ya ukaguzi, sehemu kubwa tukaona taasisi hii ilikuwa haiendeshwi sawasawa kulikuwa na mambo yanafanyika kinyume cha matakwa ya kanuni za fedha, mfano malipo ambayo milioni 3.5 ambazo zilifanywa bila kuidhinishwa na katibu mkuu na muweka hazina kati ya kipindi cha mwaka 2011 na 2016. Kulikuwa na usimamizi usio faa katika miradi ya uwekezaji wa benki ya waalimu na mwalimu house, huwezi kuona umiliki wa moja kwa moja kati ya taasisi ya waalimu na taasisi nyingine,” amesema.
Ripoti ya CAG yabaini ufisadi CWT na NIDA
Reviewed by Zero Degree
on
3/27/2018 11:15:00 AM
Rating: