Loading...

Serikali yasikia kilio cha Roma Mkatoliki

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe na Naibu wake, Juliana Shonza (katikati mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii hao baada ya kuongea na wanahabari
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe na Naibu wake, Juliana Shonza, leo wametangaza kufuta adhabu ya kufungia wasanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Roma Mkatoliki na Suzan Michael maarufu kama Pretykind.

Akizungumzia hilo, Waziri Mwakyembe alisema kuwa muda wowote kuanzia sasa Roma Mkatoliki atakuwa huru kufanya shughuli zake za muziki kama ilivyokuwa awali kwa sharti moja la kukamilisha taratibu za kujisajili BASATA.

Mwanzoni mwa mwezi Machi, mwaka huu, serikali kupitia Wizara ya Habari ilitangaza kumfungia miezi sita msanii Roma Mkatoliki kutojihusisha na masuala ya muziki kwa kukaidi amri ya kubadilisha baadhi ya mashairi ya wimbo wake wa Kiba100.

Suzan Michael maarufu kama Pretykind naye alipewa nafasi ya kuongea na wanahabari ambapo alitoa pongei kwa serikali kwa kumfundisha malezi mema na kuwaasa wasanii wenzake kuwa na tabia nzuri.
Serikali yasikia kilio cha Roma Mkatoliki Serikali yasikia kilio cha Roma Mkatoliki Reviewed by Zero Degree on 3/29/2018 05:25:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.