Loading...

Serikali yatoa neno kufuatia tukio la kushambuliwa kwa afisa ubalozi wa Syria

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abasi
Baada ya kuwepo kwa taarifa kupitia mitandao ya kijamii kuhusu kushambuliwa kwa afisa wa ubalozi wa Syria nchini Tanzania na watu watatu wasiojulikana na kupigwa ikiwa pamoja na kuporwa pesa, simu na gari aliyokuwa akiitumia kwa shughuli za ubalozi.

Kufuatia taarifa hizo Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hassan Abasi amefunguka na kukiri kupata taarifa hizo na kudai kuwa serikali inafuatilia suala hilo na itatoa taarifa kamili kuhusu jambo hilo.


"Umma unaarifiwa kuwa vyombo vya dola vinafuatilia taarifa za Afisa Ubalozi wa Syria nchini kushambuliwa, kuporwa. Taarifa kamili itatolewa" alisema Abasi. 

Aidha katika taarifa za awali zinadai kuwa afisa huyo amelazwa katika hospitali ya Agha Khan akipatiwa matibabu kufuatia shambulio hilo
Serikali yatoa neno kufuatia tukio la kushambuliwa kwa afisa ubalozi wa Syria Serikali yatoa neno kufuatia tukio la kushambuliwa kwa afisa ubalozi wa Syria Reviewed by Zero Degree on 3/20/2018 06:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.