Mugabe hatarini kunyimwa marupurupu yake
Chama tawala cha Zanu PF kimesema Robert Mugabe anaweza kupoteza kinga ya kutoshtakiwa pamoja na marupurupu kama mkuu wa zamani wa nchi ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kwenye chama.
Haya yamekuja baada ya Mugabe wiki iliyopita kuwaambia waandishi wa habari kwamba Rais Emmerson Mnangagwa amewekwa madarakani na jeshi na hivyo anatawala kinyume cha sheria.
Mbali na maoni yake kwa waandishi wa habari wa kimataifa Alhamisi iliyopita, Mugabe pia alikosolewa kwa hatua yake ya kufanya mkutano wiki mbili zilizopita na waziri wa zamani, Ambrose Mutinhiri, ambaye sasa anaongoza chama cha upinzani cha National Patriotic Front (NPF).
- Soma na hii - Marupurupu aliyopewa Mugabe kama mafao ya kustaafu
"Zanu-PF itatakiwa kukutana ili kujadili maendeleo haya mapya ... kupitia upya kama bado ni muhimu au la kwake (Mugabe) kuendelea kufurahia heshima tuliyompa," katibu wa masuala ya kisheria katika chama, Paul Mangwana aliliambia gazeti la serikali la Herald.
Mugabe hatarini kunyimwa marupurupu yake
Reviewed by Zero Degree
on
3/20/2018 05:50:00 PM
Rating: