Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 29 Machi, 2018
Arturo Vidal |
Gareth Southgate alimuonya Dele Alli wakati wa mazoezi aongeze bidii kabla hajaamua kumuacha nje ya mipango yake.
Julian Dicks anasema kuwa mashabiki wa West Ham wanahaki ya kufanya maandamono.
Arsenal inafikiria kumsajili beki wa klabu ya freiburg, Caglar Soyuncu, ambaye anakadiriwa kuwa na thamani ya pauni 30m achukuea nafai ya Per Mertesacker, ambaye anastaafu mwishoni mwa msimu. (Sun)
Hatima ya Eden Hazard katika klabu ya Chelsea inaweza kutegemeana na kama timu hiyo itafuzu kwenda Ligi ya Mabingwa au la.
Kocha wa timu ya taifa ya Senegal, Aliou Cisse amesema kuwa timu yake inalenga kuweka historia mpya kwenye Kombe la Dunia 2018.
Gabriel Jesus anatarajiwa kusaini mkataba mpya na klabu ya Manchester City licha ya kukataa kufanya mazungumzo ya kuongeza mkataba wake hivi karibuni. (ESPN)
Justin Kluivert |
Justin Kluivert anasema kuwa ndoto zake ni kufuata nyayo za baba yake mzazi na kuichezea klabu ya FC Barcelona.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Urusi, Fyodor Smolov anataka kujiunga na klabu ya West Ham kabla Kombe la Dunia halijaanza kwenye majira ya joto.
Rais wa klabu ya PAOK ya Ugiriki amefungiwa kwa miaka mitatu kwa kuvamia uwanjani akiwa na bastola. (Sky Sports)
Jordan Pickford atakuwa golikipa namba moja wa timu ya taifa ya Uingereza kwenye Kombe la Dunia.
Carlo Ancelotti anajiondoa kwenye uwezekano wa kurejea kuino moja kati ya timu kubwa kwenye EPL baada ya kueleza kwamba anaweza kwenda kuwa kocha wa timu ya taifa ya Italia.
Wakala wa Jurgen Klopp anasema kuwa meneja huyo wa Liverpool anaweza kuwa mtu sahihi wa kuinoa Bayern Munich lakini hafikirii kuondoka Anfield.
Kiungo wa klabu ya Napoli, Jorginho amejibu kitendo cha kocha wa Manchester City, Pep Guardiola kusifia uwezo wake kwa kusema kuwa anaamini anaweza kuimudu Ligi hiyo ya Uingereza. (Mirror)
Paul Lambert amemwambia aliyekuwa kiungo wa klabu ya Barcelona, Ibrahim Afellay akae mbali na Stoke City kuelekea mechi saba za mwisho.
Dominic Solanke |
Dominic Solanke hataki kubadili msimamo wake wa kubaki Liverpool, licha ya kutumikia msimu mwingine na maumivu ya kuwekwa benchi.
Jamaal Lascelles anasema kuwa Newcastle United lazima ifanye kila linalowezekana kumbakisha Rafa Benitez kwenye majira ya joto.
Gareth Southgate amemwambia majeruhi wa klabu ya Tottenham, Dele Alli asihofie nafasi yake kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kitakachoenda Urusi kwenye Kombe la Dunia.
Meneja mpya wa Birmingham, Garry Monk anasema kuwa anataka kuthibitisha uwezo wake kwa kuirejesha klabu hiyo kwenye Ligi Kuu. (Telegraph)
Nyota wa klabu ya Crystal Palace, Andros Townsend hataki kuikatia tamaa ndoto yake ya kushiriki Kombe la Dunia 2018.
Ashley Young yuko hatarini kuikosa mechi ya Manchester United dhidi Swansea baada ya kuumia goti wakati akiitumikia timu ya taifa ya Uingereza. (Express)
Everton iko katika hatua nzuri ya kufakiwa kumsajili kiungo Arsenal, Jack Wilshere kama ataondoka Emirates.
Golikipa wa Manchester United, David de Gea anasema kuwa anataka kuwa mshindi wa tuzo ya golikipa bora wa Ligi Kuu ya Uingereza (Golden Glove) kuwalipa fadhili mabeki wa timu hiyo kwa kumlinda. (Star)
Jayden Braaf (Mwenye ya rangi jezi nyekundu na nyeusi) |
Chelsea imeibuka kidedea kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya chipukizi wa Uholanzi, Jayden Braaf. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 15 amekataa ofa kutoka PSV, Ajax, Manchester City, Manchester Unite, Bayern Munich na kuchagua kutua Stamford Bridge.
Manchester United wanamfuatilia kwa karibu kiungo kutoka Tottenham, Nonso Madueke. (Daily Mail)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 29 Machi, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
3/29/2018 10:15:00 AM
Rating: