Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 8 Machi, 2018

Meneja wa Tottenham HotSpurs, Mauricio Pochettino
Maurcio Pochettino ndiye mkufunzi pekee kutoka Ligi Kuu ya Uingereza ambaye klabu ya PSG inamhitaji, Antonio Conte ni chaguo la pili. 

Klabu ya Manchester United bado haijampa David de Gea mkataba mpya licha ya kwamba Real Madrid inamfuatilia golikipa huyo kwa karibu. (talkSport)

Antony Martial anaweza kujiunga na klabu ya Juventus. Ripoti hizo zimetoka baada ya Pavel Nedved kuonekana akiwa na wakala wa mshambuliaji huyo wa Manchester United hotelini siku ya Jumatano kabla ya mechi ya Tottenhma na Juventus.

Iker Casillas ataondoka katika klabu ya FC Porto mwishoni mwa msimu huu na ripoti zinadai anaweza kutua kwenye Ligi Kuu ya Uingereza katika klabu ya Newcastle United.

Borussia Dortmund, Bayer Leverkusen na RB Leipzig zinawania saini ya kiungo wa klabu ya Red Bull Salzbug, Diadie Samassekou. (ESPN)

Graham Arnold atachukua nafasi ya Bert Van Marwijk kuiongoza timu ya Taifa ya Australia baada ya Kombe la Dunia nchini Urusi.

Hectro Bellerin, Alexandre Lacazette na Nacho Monreal wako hatarini kuukosa mchezo wa Arsenal dhidi ya AC Milan kwenye Ligi ya Europa.

Emre Can
Kiungo wa klabu ya Liverpool, Emre Can amesema kuwa hatazungumzia juu ya 
hatima yake katika klabu hiyo hadi kwenye majira ya joto. (Sky Sports)

Manchester United inatarajiwa kuanza upya mazungumzo juu ya mkataba mpya na mshambuliaji wa klabu hiyo, Anthony Martial, ambaye mkataba wake wa sasa unaisha kwenye majira ya joto mwakani.

Chipukizi wa klabu ya Lyon, Houssem Aouar anajisikia mwenye furaha baada ya Liverpool kujitokeza kutaka saini yake msimu mmoja tu baada ya kuingia katika kikosi cha timu ya wakubwa. (Star)

Paris Saint-Germain wameorodhesha majina ya makocha wanne wanaotaka wachuke nafasi ya Unay Emery baada ya kushindwa kuivusha timu hiyo katika hatua nyingine ya Ligi ya Mabingwa, akiwemo menja wa Tottenham, Mauricio Pochettino, Antonio Conte wa Chelsea, Jose Mourinho (Man United) na meneja wa Atletico Madrid, Diego Simeone. (L'Equipe)

Manchester United, Chelsea na Arsenal zinatarajiwa kushindania saini ya beki wa klabu ya Napoli, Kalidou Koulibaly kwenye majira ya joto.

Mshmabuliaji wa klabu ya Everton, Dominic Calvert-Lewin anatarajia kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kwa mara ya kwanza kwenye mechi za kirafiki dhidi ya Italy na Uholanzi.

Rekodi ya Mauricio Pochettino kuendeleza wachezaji chipukizi inamvutia beki wa klabu ya Fulham, Ryan Sessegnon kujiunga na Tottenham kwenye majira ya joto. (Mirror)

Barcelona imekatisha mazungumzo na klabu ya Gremio juu ya dili la uhamisho wa kiungo wa klabu hiyo, Arthur Melo baada ya kushindwa kukubaliana na kiasi cha pauni milioni 45 kinachohitajika kumruhusu kiungo huyo aondoke. (Sun)

N'Golo Kante
Klabu ya PSG inamtaka kiungo kutoka Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa, N'Golo Kante achukue nafasi ya Thiago Motta.

Mbali na kiungo wa klabu ya Chelsea, PSG pia inamtaka golikipa wa AC Milan, Gianluigi Donnarumma.

Brighton, Crystal Palace na West Ham zitashindana kuwania saini ya beki wa klabu ya Lille, Ibrahim Amadou kwenye majira ya joto. (Le 10 Sport)

Beki wa klabu ya Stoke City, Kevin Wimmer amewekwa chini ya amepangiwa ratiba ya mazoezi ya peke yake baada ya kuonekana hayuko 'fit' kuendena na mfumo wa meneja wa klabu hiyo, Paul Lambert.

Kiungo wa West Brom, Chris Brunt amebakiza mechi moja tu aongezewe mkataba katika klabu hiyo. (Telegraph)

Lazio inafanya mpango wa kumsajili kiungo wa Real Betis, Fabian Ruiz kwa hofu kwamba Sergey Milinkovic-Savic ataondoka klabuni hapo (Lazio) na kwenda Manchester United kwenye majira ya joto.

Golikipa wa klabu ya Liverpool, Simon Mignolet ameajiri wakala mpya kuelekea kukamilika kwa uhamisho wake wa uhakika kutoka Anfield. (Express)

Jann-Fiete Arp ataondoka Hamburg kwenye majira ya joto kama klabu hiyo itashuka daraja, huku Bayer Leverkusen na RB Leipzig zikiwa mstari wa mbelea kuwania saini yake.
 
Malcom
Jupp Heynckes amesema kuwa klabu ya Bayern Munich ina mpango wa kumsajili winga wa Bordeaux, Malcom kwenye majira ya joto. (Bild)

West Brom inatarajia kusalia na meneja wake, Alan Pardew kwa muda ujao kutokana na ugumu wa kupata mkufunzi mpya. (Daily Mail)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 8 Machi, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 8 Machi, 2018 Reviewed by Zero Degree on 3/08/2018 11:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.