Loading...

Mary Nagu akamatwa na polisi


Mbunge wa Hanang kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Mary Nagu jana aliangukia mikononi mwa Polisi baada ya kukamatwa akiwa jimboni kwake katika kijiji cha Lalaj Kata ya Lalaj wilayani Hanang.

Mh. Nagu alikamatwa majira ya saa 11:00 jioni kufuatia agizo la Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Sara Ally Msafiri kwa madai kuwa Mbunge huyo alitofautiana maagizo na mkuu huyo wa Wilaya.

Hata hivyo Mh. Nagu aliachiwa jana hiyo hiyo baada ya uongozi wa CCM Wilaya ya Hanang kuingilia kati kutafuta suluhisho la mvutano huo ambao haujaelezwa ulikuwa unahusu nini haswa.

Jitihada za kuwatafuta pande zote mbili kwaajili ya kupata ufafanuzi zaidi bado zinaendelea lakini simu zao hazipokelewi, endelea kufuatilia tutakufahamisha.
Mary Nagu akamatwa na polisi Mary Nagu akamatwa na polisi Reviewed by Zero Degree on 3/08/2018 10:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.