Loading...

Kiungo wa Real Madrid anayewindwa na Liverpool, Juventus pamoja na AS Roma

Meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp
Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali nchini Italia, bodi ya usmamizi ya klabu ya AS Roma imejaribu kuwasiliana Dani Ceballos, mwenye umri wa miaka 21, ambaye anaweza kuondoka Real Madrid kwa mkopo, baada ya msimu wake wa kwanza kama mchezaji wa klabu hiyo.

Hivi karibuni raia huyo wa Uhisapnia alieza nia yake ya kutaka kuondoka Real Madrid kwenye majira ya joto, ikiwa ni mkakati wa kusaka muda wa kutosha uwanjani akiwa na kikosi chaa kwanza.

Dani Ceballos
Ceballos alifanya mazungumzo na rais wa Madrid, Florentino Perez na kuelezea hofu yake juu ya yeye kukosa muda wa kutosha uwanjani chini ya uongozi wa Zinedine Zidane, na akaripotiwa kuwa alisema anataka kujiunga na klabu ya Liverpool ya Ligi Kuu ya Uingereza.

Nyota huyo aliyeibuka na kung'ara akiwa na klabu ya Real Betis, anawindwa na vilabu vingi ndani ya bara la Ulaya na hivi karibuni amekuwa akihusishwa na uhamisho kwenda Liverpool.

Ripoti zinadai kuwa Real Madrid tayari inatambua kwamba nyota huto anazivutia klabu nyingi, zikiwemo Liverpool, Juventus na sasa ni Roma. Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Roma, Monchi ni shabiki mkubwa wa kiungo huyo hivyo vita kubwa ya kuwania saini ya nyota huyo inatarajiwa kwenye majira ya joto.
Kiungo wa Real Madrid anayewindwa na Liverpool, Juventus pamoja na AS Roma Kiungo wa Real Madrid anayewindwa na Liverpool, Juventus pamoja na AS Roma Reviewed by Zero Degree on 3/08/2018 08:45:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.