Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 16 Machi, 2018


Hazard, Courtois na Conte wanatarajiwa kuondoka Chelsea kama klabu hiyo itashindwa kumaliza Ligi Kuu katika nafasi nne bora.

Klabu Huddersfield imethibitisha kwamba Jonas Lossl atajiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa kudumu.
 
Kwa mujibu wa Dietmar Hamann, klabu ya Bayern Munich imekuwa ikifanya mawasiliano na meneja wa klabu ya Tottenham, Mauricio Pochettino kuhusu kibarua cha kukinoa kikosi chao. (talkSport)

Beki wa Tottenham, Toby Alderweireld ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ubelgiji kitakachocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Saudu Arabia.

Mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata ameachwa nje ya kikosi cha timu yake ya taifa ya Uhispania kitakachocheza mechi za kirafiki dhidi ya Ujerumani na Argentina.

Daley Blind na Daryl Janmaat hawajaitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi kitakachocheza dhidi ya Uingereza.

Marcos Rojo
Beki wa Manchester United, Marcos Rojo amesaini mkataba mpya utakaomfanya aitumikie klabu hiyo hadi mwaka 2021. (Sky Sports)

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho ana mpango wa kuwasajili Willian na Marco Verratti kwenye majira ya joto.

Mkurugenzi wa kandanda wa klabu ya AC Milan, Massimiliano Mirabelli anasema kuwa klabu hiyo ina mpango wa kumbakisha kikosini golikipa wao Gianluig Donnarumma kwa miaka mingi zaidi. (ESPN)
 
Chelsea wanachunguza mwenendo wa kiungo wa klabu ya Arsenal, Aaron Ramsey.

Klabu ya Arsenal imepewa matumaini ya kumsajili golikipa Bayer Leverkusen, Bernd Leno baada ya Napoli kujioa kwenye kinyang'anyiro hicho.

Liverpool inatarajia kukabiliana na Arsenal kwenye mbio za kuwania saini ya nyota wa klabu ya Real Madrid, Lucas Vazquez.

Chelsea inakabiliana na ushindani mkubwa kumbakisha Eden Hazard baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa.

Klabu ya Arsenal inataka kumpa kiungo wake, Mohamed Elneny ofa ya mkataba mpya. (Mirror)

Rais kwa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez anafanya kila linalowezekana kumsajili Neymar mwishoni mwa msimu huu.
 
Aliyekuwa meneja wa Swansea, Michael Laudrup ndiye alikuwa kinara kwenye orodha ya makocha waliokuwa na nafasi kubwa ya kurithi kiti cha Luis Enrique katika klabu ya Barcelona kwenye majira ya joto mwaka jana. (Marca)
  
Meneja wa Chelsea, Antonio Conte amekiri kwamba hatima yake katika klabu hiyo haitaamuliwa na kigezo cha kama atashinda au kushindwa kutwaa taji la FA.

Marcos Alonso
Beki wa klabu ya Chelsea, Marcos Alonso amewataka wachezaji wenzake wajitume kuipatia timu yao matokeo mazuri. (Telegraph)

PSG imejiunga na Chelsea pamoja Real Madrid kwenye mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich, Robert Lewandowsk. (Le10Sport)

Olivier Giroud anasema kuwa alifanya uamuzi sahihi kuondoka Arsenal kwenda Chelsea mwezi Januari. (Independent)

Kiungo wa klabu ya PSG, Thiago Motta anaweza kuondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu. (L'Equipe)

Chelsea inatazamia kumsajili kiungo wa klabu ya Arsenal, Aaron Ramsey, ambaye mkataba wake unaisha kwenye majira ya joto.

Arsene Wenger amepata pigo jingine katika kikosi chake baada ya Laurent Koscielny kuumia katika mechi yao dhidi ya AC Milan. (Sun)

Everton inakabiliana na Liverpool kwenye mbio za kuwania saini ya straika wa klabu ya Hertha Berlin, Muhammed Kiprit, 18.

Mkufunzi wa klabu ya Borussia Dortmund, Peter Stoger ametupa lawama zote kwa Mario Gotze kufuatia timu yake kuondolewa kwenye Ligi ya Europa na Red Bull Salzbag. (Kicker)
 
Mshambuliaji wa Manchester United, Anthony Martial ameripotiwa kumtuma wakala wake kwenda kufanya mazungumzo na klabu ya Juventus.

Raphael Varane
Beki wa klabu ya Real Madrid, Raphael Varane amekiri kupokea taarifa kutoka kwa Jose Mourinho.

Gareth Southgate atawapa nafasi wachezaji wa Uingereza kuchagua kujitoa kwenye Kombe la Dunia kama wanahofia kusafiri kwenda Urusi. (Express)

Marcos Alonso ana lengo la kuzungumza na bodi ya Chelsea kuhusu sera yao ya usajili wa wachezaji kufuatia kutolewa kwao kwenye Ligi ya Mabingwa. (Star)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 16 Machi, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 16 Machi, 2018 Reviewed by Zero Degree on 3/16/2018 12:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.