Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 9 Machi, 2018

Ikiwa ktaika uwanja wa nyumbani, AC Milan ilikubali kichapo cha goli 2-0 kutoka kwa Arsenal
Mkufunzi wa AC Milan, Gennaro Gatuso amesema kuwa timu yake haikucheza kwa ummoja katika mchezo wao dhidi ya Arsenal kwenye Ligi ya Europa.

Liverpool inaongoza mbio za kuwania saini ya nyota wa Monaco na timu ya taifa ya Ufaransa, Thomas Lemar. (ESPN)

Meneja wa klabu ya Fulham, Slavisa Jokanovic ameibuka ghafla na kuwa mmoja wa wanaowania kuinoa Chelsea kama Antonio Conte ataondoka kwenye majira ya joto.

Paris Saint-Germain watazungumza na Conte juu ya uwezekano wa kuichukua nafasi ya Unai Emery kama kibarua chake katika Ligi Kuu ya Uingereza kitaisha.

Barcelona imezionya klabu za Ligi Kuu ya Uingereza kuwa iko tayari kusajili wachezaji wengi chipukizi kutoka Uingereza. (Daily Mail)

Bayern Munich imeingia kwenye mbio za kuwania saini ya straika wa klabu ya Bordeaux, Malcom.

Mshambuliaji wa Leicester City, Riyad Maahrez anakiri kujutia sakata la baada ya uhamisho wake kwenda Manchester City kugoma lakini anasisitiza kuwa kwa sasa akili yake imetulia sehemu mmoja. (Sky Sports)

Gareth Southgate anatarajiwa kumfanya mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane kuwa nahodha wake wa Timu ya Taifa ya Uingereza kwenye Kombe la Dunia nchini Urusi wakati wa majira ya joto.

Berke Ozer
Chelsea wanatazamia kumsajili golikipa kutoka Uturuki, Berke Ozer achukue nafasi ya Thibaut Courtois. (Star)

Steven Gerrard amedai kuwa winga wa klabu ya Liverpool, Mohamed Salah ni zaidi ya Didier Drogba, Toure na Okocha. (talkSport)

Nyota wa klabu ya Barcelona, Denis Suarez yuko hatari kuikosa mechi ya marudio dhidi ya Chelsea kwenye Ligi ya Mabingwa wiki ijayo baada ya majeruhi.

Fulham inakabiliana na ushindani kutoka Anderlecht katika kuwania saini mshambuliaji wa klabu ya Newcastle, Aleksander Mitrovic. (Mirror)

Harry Kane amesema atasalia katika klabu ya Tottenham kwa walau msimu mmoja au zaidi.

Manchester United inafanya mipango ya kuwanasa mabeki wawili kutoka klabu ya Tottenham, Danny Rose na Toby Alderweireld kwenye majira ya joto.

Ripoti zinadai Tottenham inamfukuzia beki wa klabu ya Stuttgart, Benjamin Pavard.

Yasin Ben El-Mhanni
Newcastle iko tayari kumruhusu mchezaji wake, Yasin Ben El-Mhanni aondoke mwishoni mwa msimu huu. (Sun)

Kiungo wa klabu ya Liverpool, Emre Can anasita kukubaliana na uhamisho kwenda Juventus kwa kuwa anahisi Real Madrid inaweza kujitokeza kutaka kumsajili kwenye majira ya joto. (Express)

Meneja wa Juventus, Massimiliano Allegri anasisitiza kwamba hatajiunga na Ligi Kuu ya Uingereza kwenye majira ya joto kama inavyodaiwa.

Phil Neville anataka timu ya taifa ya Uingereza ya wanawake ipewe haki sawa na ile ya wanaume baada ya kudai kuwa walilazimka kusafiri katika mazingira ya hali duni.

Sam Allardyce amekiri kuwa atafukuzwa kazi katika klabu ya Everton isipokuwa kama matokeo ya klabu hiyo yatabadilika. (Times)

Yohan Benalouane
Beki wa Leicester, Yohan Benalouane anaweza kuikabili Uingereza kwenye Kombe la Dunia baada ya kuweka wazi utayari wake wa kuichezea timu ya taifa ya Tunisia. (Guardian)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 9 Machi, 2018  Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 9 Machi, 2018 Reviewed by Zero Degree on 3/09/2018 10:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.