Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 17 Machi, 2018

Robert Lewandowsik
Real Madrid wamefikia makubaliano binafsi na mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich, Robert Lewandowsik.

Pele ana amini Tite anafaa kuiongoza timu ya taifa ya Brazil kwenye Kombe la Dunia nchini Urusi.

Beki wa Atletico Madrid na Brazil, Luiz Filipe yuko hatarini kulikosa kombe la dunia baada ya kuvunjika mfupa. (ESPN)

Alan Pardew alifanya mazungumzo na bodi ya West Brom kuhusiana na hatima yake katika klabu hiyo ya Uingereza.

Tottenham inatarajia kufanya mazungumzo na Heung-Min Son juu ya kandarasi mpya. (Sky Sports)

Paul Pogba na Antony Martial wanaweza kulazimisha uhamisho wao kuondoka Old Traford kama Mourinho ataendelea kuwa meneja wa Man United.

FIFA imeidhinisha kutumika kwa teknolojia ya VAR kwenye Kombe la Dunia nchini Urusi. (talkSport)

Beki wa Real Madrid, Raphael Varane amethibitisha kwamba Manchester United ina nia ya kumsajili.

Kiungo wa klabu ya West Ham, Domingos Quina anawindwa na Borussia Dortmund. (Sun)

Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte ameanza kuonyesha dalili za kutaka kuondoka Stamford Bridge. (Daily Mail)

Jack Wilshere
Everton wamejiandaa kumlipa Jack Wilshere pauni milioni 8 kama ada ya usajili kumshawishi atue Goodison Park kwenye majira ya joto.

Brentford wanatarajia kupokea bonasi ya pauni milioni 1 kama malipo kutoka Burnley baada ya James Tarkowski kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza wiki hii.

Watford wanakataa kulipa fidia kwa Marco Silva, licha ya kuwa meneja huyo kutishia kuwachukulia hatua za kisheria. (Times)

Juventus imeripotiwa kukutana na mawakala wa Anthony Martial, huku klabu hiyo ikijiandaa kutoa ofa kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji huyo kutoka Man United.

Wolves wana matumaini ya kuipiku Arsenal kwenye mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa klabu ya AC Milan, Andre Silva kama watafanikiwa kupanda daraja.

Leroy Sane ana amini Manchester City inaweza kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa kama itafanikiwa kupita kwa Liverpool. (Mirror)

Meneja wa Chelsea, Antonio Conte ana uhakika hakutakuwa na wachezaji nyota wataotaka kuondoka kama timu yake itashindwa kumaliza Ligi Kuu katika nafasi nne bora.

Michael Appleton anapewa nafasi kubwa ya kuweza kuchukua madarka ya kuinoa West Bromwich Albion kwenye majira ya joto. (Telegraph)

Kwa mujibu wa neneja wa Valencia, ni bora Manchester United ingemsajili Geoffrey Kondogbia kuliko Paul Pogba.

Alvaro Morata
Meneja wa timu ya taifa ya Uhispania, Julen Lopetegui anategemea kuona mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata akiwa na mwisho mzuri kwenye Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu. (Express)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 17 Machi, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 17 Machi, 2018 Reviewed by Zero Degree on 3/17/2018 10:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.