Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 24 Machi, 2018
David de Gea |
David de Gea ameomba kwa siri kuondoka Manchester United baada ya kufanya mazungumzo na wawakilishi wa klabu ya Real Madrid.
Beki wa Liverpool, Joel Matip anasema kuwa anatamani kuongeza idadi ya magoli kwenye hesabu yake baada ya kuona wachezaji wenzake wakifunga magoli ya bure msimu huu. (Star)
Manchester United iko hatarini kumkosa Gareth Bale kwenye majira ya joto kwa sababu ya mambo ambayo Jose Mourinho anamfanyia Luke Shaw, ambaye yuko chini ya wakala anayemsimamia raia huyo wa Wales.
Patrick Kluivert anataka mtoto wake, ambaye ni mshambuliaji wa Ajax, Justin, aachane na uhamisho kwenda Manchester United na afuate nyayo zake kwa kujiunga na Barcelona.
Cristiano Ronaldo anataka kuhakikisha analipwa euro milioni 1 zaidi ya Lionel Messi au Neymar kabla ya kukubali kusaini mkataba mpya Real Madrid.
Andrea Pirlo atakuwa sehemu ya benchi la ufundi la timu ya taifa ya Italia kama kati ya Carlo Ancelotti au Antonio Conte watateuliwa kama meneja kwenye majira ya joto.
Rangers wana nia ya kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Motherwell, Louis Moult baada ya nyota huyo kuhsindwa kuonyesha makali yake akiwa na klabu ya Preston North End. (Daily Mail)
Wakala wa Hector Bellerin anasema kuwa anafurahia kuwa katika klabu ya Arsenal na wala si Manchester United au Juventus wameshajitokeza kupeleka ofa ya kutaka kumsajili.
Bayern Munich wataelekeza nguvu yoa kwa mshambuliaji wa RB Leipzig, Timo Werner au wa Tottenham, Harry Kane kama Robert Lewandowski atalazimisha kuondoka kwenye majira ya joto.
Martin Dubravka |
Golikipa wa klabu ya Sparta Prague anayeichezea Newcastle kwa mkopo, Martin Dubravka yuko tayari kusaini mkataba wa kudumu na klabu hiyo ya Uingereza kama itaepukana na kushika daraja.
Mshambuliaji wa klabu ya FC Basel, Mohamed Elyounoussi amemtaka Arsene Wenger amsajili baada ya skauti wa Arsenal kumchunguza kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester City.
Willy Cabellero atabakia kuwa kama golikipa namba mbili wa klabu ya Chelsea msimu ujao, bila kujali kama Thibaut Courtois atabaki au ataondoka klabuni.
Real Madrid wanapanga kujaribu kumsajli Marcus Rashford kutoka Manchester United kwenye majira ya joto, ikiwa ni mipango yao ya kupunguza wastani wa umri wa wachezaji ndani ya kikosi chao. (Sun)
Kocha mkuu wa Borussia Dortmund, Peter Stoger anasema kuwa Usain Bolt bado ana kazi kubwa ya kufanya ili afanikiwe kuwa mchezaji wa kimataifa.
Meneja mpya Oxford United, Karl Robinson anasema kuwa aliachana na klabu ya Charlton kwa sababu binafsi.
Sergio Aguero ameachwa nje ya kikosi cha timu ya taifa ya Argentina ambacho kitacheza dhidi ya Uhispania Jumanne. (Sky Sports)
Hatua ya mwisho ya mkakati wa miaka 3 uliopangwa na La Galaxy kumshawishi Zlatan Ibrahimovic ajiunge nao ilikuwa ni kupanga mkutano wa pamoja na David Beckham kwa chakula cha usiku. (Times)
Nyota anayewaniwa na klabu ya Liverpool, Dani Ceballos amekiri kuwa 'future' yake katika klabu ya Real Madrid haieleweki baada ya kutokea kwenye michezo 19 tu tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea Real Betis kwenye majira ya joto.
Julian Draxler |
Winga anayewindwa na klabu ya Arsenal, Julian Draxler ameonyesha mapenzi yake kwa Real Madrid na anafanya kila linalowezekana kufanikisha uhamisho wake kwenda Uhispania kutoka PSG.
Ryan Giggs amemwambia Gareth Bale kuwa ni bora zaidi akaendelea kubaki Real Madrid, licha ya kushawishika kurejea Ligi Kuu ya Uingereza. (Express)
Meneja wa klabu ya Everton, Sam Allardyce anasema kuwa alikuwa akitamani kumpata Jack Wilshere siku zote.
Wachezaji wenzake na Gareth Bale kutoka timu ya taifa ya Wales wana amini atajiunga na Manchester United kama Zinedine Zidane atabakia kuwa mkufunzi wa Real Madrid msimu ujao.
Vincent Kompany ana amini kuwa hata mashabiki wa Man United watakuwa wanaishangilia Manchester City wakati itakapokuwa inacheza dhidi ya Liverpool kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa. (Mirror)
Ryan Giggs anasema kuwa alifanya mazungumzo ya kina na Eddie Jones pamoja na Antonio Conte kabla hajaamua kuingia kwenye kazi ya ukufunzi katika ngazi ya kimataifa akiwa na Wales. (Telegraph)
Antoine Griezmann |
Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann anasema kuwa ataamua juu ya hatima ya uhamisho wake kabla ya Kombe la Dunia kwenye majira ya joto. (Independent)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 24 Machi, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
3/24/2018 11:31:00 AM
Rating: