Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 6 Machi, 2018

Arsene Wenger akiongea na Mikel Arteta mazoezini 
Nyota wa klabu ya Arsenal hawataki Mikel Arteta achukue nafasi ya Arsene Wenger kama meneja wao mpya.

Mauricio Pellegrino anakabiliana na kutimuliwa kazi mwishoni mwa msimu huu hata kama Southampton haitashuka daraja.

Hector Bellerin amekasirikia kitendo cha meneja wa Arsenal, Arsene Wenger kumuacha nje ya kikosi cha klabu hiyo masaa mawili kabla ya kufungwa goli 2-1 na Brighton.

Nafasi ya Arsene Wenger katika klabu ya Arsenal iko inafanyiwa uchunguzi katika misingi ya mechi moja baada ya nyingine.

Aliyekuwa nyota wa klabu ya Chelsea, Ramires anakiri kwamba anataka kurejea Stamford Bridge.

Arsenal inataka atakayerithi nafasi ya Arsene Wenger awe kocha mwenye uwezo wa kumaliza enzi za utawala wa makocha wote wenye nguvu. (Sun)

Mkurugenzi mkuu wa klabu ya West Brom, Mark Jenkins pamoja na wamiliki wa klabu hiyo watajadili juu ya hatima ya Alan Pardew kama meneja wa klabu ya hiyo nchini China.

Fiorentina pamoja na Cagliari wameistaafisha jezi namba 13 iliyokuwa ikitumiwa na Davide Astori kufuatia kifo cha nahodha huyo, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 31.
Pep Guardiola anasisitiza kuwa, klabu ya Manchester City bado haijafikia hatua ya kulinganishwa na FC Barcelona. (Sky Sports)

Christian Pulisic
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez anataka kumsajili winga wa Borussia Dortmund, Christian Pulisic anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 80 achukue nafasi ya Gareth Bale katika dimba la Santiago Bernabeu. (Diario Gol)

Bayern Munich inataka kumsajili beki wa klabu ya FC Porto, Diogo Dalat kwa mtazamo wa kutaka atumie mwaka mmoja au zaidi chini ya Rafinha ajifunze utaratibu kabla ya kupewa madaraka ya kudumu. (Kicker)

Wachezaji wa Chelsea wanahofia meneja mkuu wa timu hiyo, Antonio Conte anaweza kusababisha Eden Hazard aondoke Stamford Bridge kwa mbinu za kuupa kipaumbele usalama wa mchezaji.

Jurgen Klopp amekiri kuwa Liverpool ilifanya makosa kumrejesha Adam Lallana uwanjani kwa haraka mwanzoni mwa msimu huu. (Telegraph)

Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Eden Hazard anasita kusaini mkataba mpya na klabu hiyo kwa matumaini ya kwamba Real Madrid inaweza kurejea sokoni kuwania waini yake.

David Beckham anasisitiza kuwa Phil Neville ni mkufunzi sahihi kwa timu ya taifa ya wanawake ya Uingereza. (Daily Mail)

Matumaini ya Arsene Wenger kubakia kibaruani ni kikwazo kwa Arsenal kwa klabu hiyo kutwaa taji la Europa Ligi. (Star)

Atletico Madrid imeungana na klabu ya Tottenham, Arsenal, na Barcelona kwenye mbio za kuwania saini ya kiungo wa klabu ya Sahlke 04, Max Meyer, ambaye mkataba wake na klabu hiyo ya Ujerumani utaisha kwenye majira ya joto. (Bild)

Mousa Dembele
Mousa Dembele anatazamia ushindi Tottenham kwenye Ligi ya Mabingwa ili kulipa fadhila kwa meneja wa klabu hiyo, Mauricio Pochettino baada kuwa amemfananisha na Diego Maradona.

Ilkay Gundogan anahofia Manchester City inaweza kupoteza mwamko kwenye Ligi ya Mabingwa kama itatwaa taji la Ligi Kuuya Uingereza mapema.

Cesar Azpilicueta amewaonya wachezaji wenzake wa Chelsea kuwa wanatakiwa wasiruhusu mchezo mwingine upotee kama wanataka kumaliza ligi katika nafasi nne bora. (Mirror)Wawakilishi kutoka Gremio walikuwa Barcelona jana Jumatatu kwa lengo la kukamilisha dili la uhamisho wa Arthur kwenda Nou Camp kwenye dirisha la usajili mwezi Januari 2019. (Marca)

Mario Balotelli anasema kwamba yuko tayari kurejea katika Ligi Kuu ya Italia (Serie A) na angependelea kujiunga na Napoli au Juventus.

Klabu ya Barcelona inatazamia kumsajili beki wa Arsenal, Hector Bellerin, wakati Manchester City ikivizia saini ya kiungo wa klabu ya Napoli, Jorginho. (ESPN)

Arsene Wenger anaamini kuwa yeye pekee ndiye anayeweza kuifanya Arsenal isonge mbele na ameliambia benchi la ufundi kwamba, klabu hiyo italazimika kumfukuza kazi kuweka kikomo cha utawala wake wa miaka 22. (Times)

Garry Monk amesema kuwa atatumia uzoefu wake alioupata kutoka Leeds United kuiongoza Birmingham City baada ya kuwa meneja wa tano wa klabu hiyo ndani ya miezi 12. (Guardian)

Aliyekuwa meneja wa Hull City, Phil Brown ametuma maombi ya kazi ya umeneja katika klabu ya Swindon Town. (Express)

Mkufunzi wa sasa wa klabu ya PSG, Unai Emery
Mmiliki wa klabu ya PSG, Nasser Al-Khelaifi anataka Zinedine Zidane achukue nafasi ya Unai Emery mwishoni mwa msimu huu kama Real Madrid itaamua kuachana na Mfaransa huyo. (Le10Sport)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 6 Machi, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 6 Machi, 2018 Reviewed by Zero Degree on 3/06/2018 12:22:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.