Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 27 Machi, 2018

Isco
Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola anatazamia kufanya uvamizi katika kikosi cha Real Madrid na pauni milioni 75 mkononi kusaka saini ya Isco kwenye majira ya joto.

Manchester United inaweza kuachana na karibu wachezaji tisa wa kikosi cha kwanza mwishoni mwa msimu.

Uamuzi wa Gareth Southgate kumchezesha Kyle Walker kama beki wa kati ulikuja baada ya kocha huyo kufanya mazungumzo na meneja wa Manchester City, Pep Guardiola.

Eliaquim Mangala amepokea Medali ya ushinda wa Taji la Carabao kutoka klabu ya Manchester City licha ya kuwa Everton kwa mkopo.

Meneja wa klabu ya Huddersfield, David Wagner yuko kwenye mazungumzo ya kandarasi mpya na klabu hiyo, huku kukiwa na tetesi nyingi zinazozungumzia mstakabali wa maisha yake kisoka.

Norwich wanataka kiasi cha pauni milioni 25 kumwachia kiungo wao, James Maddison. (Sun)

Eden Hazard amesema kuwa atacheza sehemu ambayo Antoni Conte atahitaji na kuongeza kwamba, hana shida na kitendo cha Mutaliano huyo kumchagulia nafasi ya kucheza uwanjani.

Chaguo la kwanza kwa aliyekuwa meneja wa Borusia Dortmind, Thomas tuchel ni Bayern Munich na sio Arsenal.

Kiungo wa klabu ya Arsenal, Mohamed Elneny amesaini mkataba mpya katika klabu hiyo.
 
Emre Can amekanusha taarifa zinazodai anahitaji kiasi kikubwa cha mshahara ili akubali kubaki Liverpool. (Sky Sports)

Barcelona inapanga kushtukiza usajili wa Luke Shaw kufuatia beki huyo wa Man United kutofautiana na Jose Mourinho.

Gareth Southgate atafanya mabadiliko ya kikosi chake kwenye mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Itali Jumaane kwa sababu anaogopa majeruhi kablaya Kombe la Dunia.

Kieran Tierney
Manchester United wanaendelea kuongeza juhudi kwenye mchakato wao wa kumsajili beki wa klabu ya Celtic, Kieran Tierney anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 25.

Steve McClaren hana mpango na kibarua katika klabu ya Scunthorpe baada ya kuamua kusubiri hadi mwishoni mwa msimu kabla hajajiunga na klabu yoyote.

Ronaldinho amesema kuwa yalibakia masaa 48 ajiunge na klabu ya Manchester United mwaka 2003 kabla uhamisho huo kushindikana. (Mirror)

David de Gea amesma kuwa ataitolea nje klabu ya Real Madrid na badala yake atachagua kubaki Manchester United. (talkSport)

Arsenal wamechukizwa na kitendo cha Uingereza kumpa wakati mgumu Jack Wilshere wakati alipokuwa pamoja na timu ya taifa.

Meneja wa Huddersfield, David Wagner atachelewa kufanya maamuzi juu ya hatima yake katika klabu hiyo hadi mwisho wa msimu, huku kukiwa na ripoti zinazomhusisha na uhamisho kwenda Southampton. (Star)

Liverpool wana wasiwasi kuwa majeraha Joe Gomez katika kifundo chake cha mguu yanaweza kumweka nje nyota huyo kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester City.

Daniel Sturridge
Daniel Sturridge amerejea mazoezini katika klabu ya West Brom kufuatia majeraha katika paja.

Peter Beardsley yuko kwenye orodha ya VIP kwenye dimba la Wembley kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa Uingereza dhidi ya Italia licha kuwa chini ya uchungzi Newcastle kwa tuhuma za uonevu na ubaguzi. (Daily Mail)

Kama Lewis Cook atafanikiwa kucheza mechi yake ya kwanza katika timu ya taifa ya Uingereza katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Italia, babu yake atajipatia kiasi cha pauni 17,000.

Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) linapanga kufanya ukaguzi wenye lengo la kuipesha timu ya taifa ya Uingereza na mechi ya kirafiki Ijumaa usiku kufuatia shida iliyojitokeza Amsterdam. (Telegraph)

Uingereza itakuwa na mechi moja tu kujiandaa na mpira wa Kombe la Dunia kwa sababu ya ahadi za kibiashara kati ya FA na Kampuni ya Nike.

Chipukizi wa klabu ya Fulham, Ryan Sessegnon atacheza mchezo wake wa kwanza katika timu ya taifa ya Uingereza U21 dhidi ya Ukraine. (Times)

Scott McTominay
Scott McTominay hakusafiri pamoja na timu ya taifa ya Scotland kwa sababu ya baada maumivu ya misuli. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 27 Machi, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 27 Machi, 2018 Reviewed by Zero Degree on 3/27/2018 10:18:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.