Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 18 Machi, 2018

Julian Draxler
Jurgen Klopp anajaribu kuishawishi bodi ya Liverpool kumsajili kiungo wa klabu ya Paris Saint-Germain, Julian Draxler mwishoni mwa msimu huu.

Arsenal wanajaribu kufanya mazungumzo na Robert Lewandowski, ambaye anataka kuondoka Bayern Munich baada ya miaka minne lakini mshambuliaji huyo anaitamani Real Madrid. (Express)

Real Madrid na PSG zitashindania saini ya mshambuliaji wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Argentina, Paulo Dybala. 

Mshambuliaji wa Cagliari, Han Kwang-song anayewindwa na Tottenham bado anatamani kujiunga na klabu ya Juventus, licha kwamba klabu hiyo ya Italia ilishindwa kutimiza ahadi yake ya kumsajili mwezi Januari. (Calciomercato)

Nyota wa klabu ya Sunderland amekamatwa na polisi akidaiwa kuendesha gari akiwa amelewa na kusababisha ajali.

Gianluig Buffon ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Italia kucheza mechi za kirafiki dhidi ya Uingereza na Argentina, licha ya kustaafu soka la kimataifa mwaka jana. (Sky Sports)

Luis Enrique ana matumaini Arsenal itamteua kuwa meneja wao mpya achukue nafasi ya Arsene Wenger kwenye majira ya joto.

Fred
Manchester United iko mbele ya Manchester City kwenye mbio za kuwania saini ya kiungo wa Shakhtar Donetsk, Fred. (Star)

Kiungo wa klabu ya Arsenal, Jack Wilshere anataka kulipa fadhila kwa meneja wa Uingereza, Gareth Southgate kwa kumita kikosini. (Independent)

Zinedine Zidane amekanusha taarifa zinazodai kuwa Gareth Bale hafurahii kuwa Real Madrid.

Gareth Southgate ameapa kuipeleka familia yake kwenye Kombe la Dunia nchini Urusi licha ya kuhofia usalama. (Daily Mail)

Paris Saint-Germain imehamishia mapenzi yake kwa meneja wa klabu ya Juventus, MassimilianoAllegri.

AC Milan itaka kuongeza mkataba wa Gennaro Gatuso katika dimba la San Siro baada ya kuingo huyo aliyeichezea klabu hiyo kuonyesha uwezo mkubwa tangu achukue madaraka ya kukinoa kikosi chao. (Gazzetta dello Sport)

Wakala wa Paul Pogba, Mino Raiola anamuuza kiungo huyo wa Manchester United kwa watakaomhitaji baada ya kutofautiana na Jose Mourinho.

Liverpool wanakabiliana na ushindani kutoka Real Madrid kwenye mchakato wa  kumsajili golikipa wa Roma, Alisson baada ya klabu hiyo ya Uhispania kuanza mkakati wa kutaka kuvunja rekodi kwa kumsajili mlinda mlango huyo kwa kiasi cha pauni milioni 70 kwenye majira ya joto.

West Ham, Watford na Newcastle zitashindania saini ya kiungo wa Fulham, Tom Cairney, ambaye ataruhusiwa kuondoka kwa adya ya pauni miloni 20.

Marcus Rashford na Harry Kane
Marcus Rashford anasema kuwa yuko tayari kuwa mshambuliaji tegemezi wa timu ya taifa ya Uingereza kwenye Kombe la Dunia kama Harry Kane hatakuwa fit kukiungoza kikosi cha Gareth Southgate. (Mirror)

Neymar anataka mshahara wa pauni milioni 1 kwa wiki abaki Paris Saint-Germain, huku Real Madrid ikiwa na matamanio makubwa ya kumsajili.

John Terry anataka kuichezea Aston Villa hadi msimu ujao hata kama atakuwa adui wa klabu yake ya zamani Chelsea kwenye Ligi Kuu ya Uingereza. (Times)

Arsenal iko tayari kuliia pauni milioni 53 kumnasa Luka Modric kutoka Real Madrid kwenye majira ya joto.

Zinedine Zidane anataka kutibua dili la Juventus kwa kujaribu kumsajili Emre Can, ambaye mkataba wake na klabu ya Liverpool utaisha mwishoni mwa msimu huu.

Tottenham itaanza mazungumzo ya mkataba mpya na Heung-Min Son kama zawadi kwa starika huyo kufuatia kiwango alichokionyesha msimu huu.

Andre Silva
Wolves itaikabili Arsenal kwenye mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa AC Milan, Andre Silva ambaye amefanikiwa kufunga goli moja tu tangu ajiunge na klabu hiyo ya Italia kwa pauni milioni 34 kwenye majira ya joto. (Sun)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 18 Machi, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 18 Machi, 2018 Reviewed by Zero Degree on 3/18/2018 11:25:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.